Huyo jamaa ni aina ya wanaume aliowasema Bishanga,ila sio WANAUME aliowasema Aspirin,huyo jamaa hajiamini kabisa na hafai kuitwa mwanaume,hebu huyo binti akutane na MWANAUME kama mimi,lazima kwa kuunganisha nguvu tungekua na mjengo kama wa NSSF!!
Mkuu si ulisikia walipika na kupakua huko tabata!
Habari zenu wapendwa,
Kuna mkaka ni mkazi wa dar ila anafanya kazi mgodini huko mwanza huku anakuja kila baada ya miezi miwili,Alikutana na mdada huko mwanza Mdada anafanya kazi huku dar kule alienda kikazi,wakapeana kontakt, na mawasiliano yakaendelea na wakawa wapenzi.
Kwa kipindi cha miezi minne ya mahusiano yao hakuna aliyekua anajua kwa mwenzie,basi wakapanga jamaa atakapokuja dar wakaoneshane makwao,basi jamaa akarudi dar ijumaa iliyopita km kawa wakakutana na jmosi jamaa kampeleka mdada kwake tabata wakashinda huko wakapika na kupakua.
Jpili mdada naye akampeleka jamaa kwake maeneo ya Sinza hapo ndio balaa lilipoanzia kwan muda wote wakiwa pale yule mkaka alikuwa hana raha mwenzie akamuliza kulikon mbona ulikuja vizuri,yy akamuuliza pale anaishi na nani akamwambia mbona nilishakwambia naishi peke yangu.
Akamwomba amwonyeshe slip yake ya mshahara mdada akapigwa butwaa ila akamwonyesha kumbe kaharibu jamaa kanyanyuka na kuondoka akiwa amekasirika mdada hakumwelewa akambembeleza bila mafanikio,usiku wake jamaa akamtumia bint msg kuwa hamtaki tena,kwa sababu anahisi huyo mdada atamtawala maishani kwa vile kwanza ana kipato kikubwa,na ameshajijenga sana kimaisha,hivyo ni rahisi yeye kutokuwa na sauti ndani ya nyumba,au huyo dada anaweza kumwaga wakati wowote na kutoka na wenye uwezo km yy.
Mpaka ninavyoandika huu uzi jamaa hapokei simu na jana kaondoka kurudi mwanza,dada watu kachanganyikia alishampenda jamaa kupita kiasi hata hajui cha kufanya!
Asa mi nauliza hivi nyie wanaume hivi binti kuwa na kipato kikubwa kuliko mwanaume ni kweli ni tatizo kwenye mahusiano?
Na dada afanyaje ili jamaa aelewe na waendelee?
Wala hakuona suruali,ishu ni kwamba baada ya kuona thaman za mle ndani hakuweza kuamin gafla kuwa ni uwezo wa yule binti,
Ndio maana akataka kuthibitisha kwa kuomba slip ya mshahara ili kulinganisha na vitu anavyona mle ndani,
Na alipopata uhakika ndio akaona binti kamuacha mbali na kuamua kukimbia!
Tunarudi palepale mkuu, kulingana na maelezo yako hata wewe huamini kuwa mwanamke anaweza akakuzidi mkwanja halafu maisha yakawa poa na ndio maana ukaamua kukomaa ili angalau muwe level sawa.nimesoma uzi huu nikakumbuka mbali sana....hali hii iliwahi kunikumba mimi ila mimi sikufanya kama huyu bwana alivyofanya....mi baada ya kujua kuwa mwenzangu yuko juu sana kwa kweli ilibidi nijiongeze namna ya kufikiria na namna ya kuongea kipato......bila kumwambia wala nini nilianza kuchakalika sana a kilichorahisisha ni kwamba nilikuwa natumia usafiri wake..kwa kuwa tulikuwa tunakaa mikoa miwili tofauti...nilihakikisha kila akija anakuta maendeleo flan....nakumbuka alikuja mda flani akakuta nafuga kuku wengi sana na nimeajili mtu wa kuwahudumia akafurahi sana.....mimi kimya.....
akaja wakati mwingine nimenunua shamba na nikampeleka kwenda kuliona...kule shamba nikawa nafuga ng'ombe wa kisasa nako nikaweka mtu.....kwa kuwa tayari nilikuwa na kibanda cha kuishi nikaenda bank nikachukua mkopo wa maana..nikaenda iringa nikaaanza kusafirisha mbao naleta dar buguruni....mtaji ukakua nilifanya kazi ile kwa miezi kama 6...hakika nilipata faida kubwa sana......wakati nafanya yote haya mwenzangu nae alikuwa nashughuli zake(mabotique 3, saluni 4 zote ziko dar) nashughuli kibao na nyumba moja kapangisha......
baada ya kujiridhisha nae na kwa kuwa alikuwa na mawazo chanya kwangu nikaridhika nae sana......baada ya miaka miwili nikamvika pete na tukaunganisha mali zote aliochuma yeye na mimi ....baadae nikasafiri nikaenda kuongeza shule kidogo huko italy huku yeye akisimamia miradi yangu na yake ujenzi wa nyumba yangu na mwaka jana tar 8 september tulifunga ndoa na ndoa yetu tulifungia italy na ni kati ya ndoa zilizofungwa na baba ntakatifu Benedict wa 16......sasa tupo katika nyumba niliyojenga mimi tunaishi, nyumba alizojenga yeye wakati yuko alone zimepangishwa zote na tunaishi salama na maisha yanakwenda vizuri sana....namshukuru Mungu mama blanca alinipa changamoto nyingi sana juu ya maisha ..
kikuwa nilichokuwa nawaza ni kwamba huyu anawezaje na kwa nini mimi nishindwe!!!? na hakika kwa kiasi nilicho nacho nakwa maisha tunayoishi namshukuru Mungu....
huyu kijana mwenzangu aliyekimbia hana changamoto..hataki kujifunza na mvivu wa kujishughulisha ndo wale wanaosubiri mishahara ya kila mwezi pasipo kujishughulisha.....unakimbia mwaanamke kisa ana kipato kukuzidi?!!!
hivi Canta una ruksa maalum kumesema mkasa wa binti hapa jamvini maana sitaki baadaye urudi na manundu usijekosa mume bure! ohoo😛oa
Orayt, hata mie naamini siyo wewe. Sasa waweza kutuambia hiyo salary slip inasoma mshahara wa huyo binti ni shingapi vile?My dia kapipi co mie bwana!haa haa haa!ningekwambia tu shost tumfungie safari lol!leo cjakuona kbs,umeadimika sn!
Inawezekana kwan kila binadam ana style zake za kufanya maamuzi bila kujali ataonekana kituko au vp,hakuna kiumbe complicated kama binadamu. huwa anawaza mengi sana lakini anaweka wazi machache mno. na mara nyingi anayoyasema siyo ndiyo anayomaanisha. huyo mwanaume ana sababu nyingine kabisa tofauti na hiyo anayoisema.
ushauri kwa mwanamke ni kuwa aikubali hii hali, kwani huenda ameepushwa na jambo baya, au anaandaliwa kilicho chake kwa maisha yake. siwezi kusema huyo bwana ni mbaya au mzuri, kwani alichokifanya ni kujizuia kumwoa asiye mpenda -watu hupendana ndiyo huoana na si mmoja anapenda ndipo anaoa.ninaamini kwa 100% sababu ya kipato siyo ndiyo imemkimbiza huyu bwana. anasababu ambayo anaijua yeye, huenda tangu mwanzo hakuwa makini, sasa amaona dada yupo serious na yeye (mwanaume )hayupo tayari ndo amekuja na hizo sababu "dhaifu"
Jamaa noma...! Mke wako akiteuliwa kuwa Asha-Rose Migiro utamwacha? It's just a matter of logical thinking.
Tatizo ni kwamba nafasi ya mke na suala zima la haki ni subjective, yaani hakuna standard kwa hiyo namna wewe unavyoiangalia ndoa unaweza kuona ni sawa kabisa mke kuwa level sawa na mume lakini kwa mwingine asione sawa. Na lawyers wengi wa kike ndoa zinawashinda kwa sababu generally wanaume wengi kama sio wote wanaamini kuwa wana mamlaka juu ya mke, kitu ambacho lawyers hawakubali maana wao wanaamini ndoa ni partnership, na hapo ndio tatizo linapoanzia Upooooo?Cheo/pesa has got nothing to do with mapenzi ya wawili wapendanao!! Mnawagwaya bure tu watu wa TAMWA/lawyers, wao sanasana wamebase kwenye haki ila baadhi ya watu wanashindwa kutofautisha waambiwayo. Wengi wanashindwa kutofautisha kati ya human rights( mke) na majukumu & nafasi ya mke katika ndoa/familia yake!! Kumburuza mume ni tabia binafsi ya mtu na pengine yaweza kuwa imesababishwa na mume mwenyewe na wala sio pesa, otherwise ndoa za hivo zisingedumu!! Nakuachia mtoto huyo we endelea nae tu kwa raha zako ila chonde chonde, handle with care! Hahahahaaa am neither of such type of waburuzaji but u should avoid me lol.........najoke bana!! Mimi niko simple sana mwaya usiniogope jamani mweeh!
Tunajua kuwa sawa kwa sawa haitakaa itokee,ila sio kung'ang'ania mfumo dume,kweli lakini...but mwanaume kuwa sawa sawia na mwanamke mi sidhani kama itafika zama iyo
Kimsingi sidhani kama jamaa anafikria straight, kwanini uombe salary slip ya mwenzio?????, Pili jamaa amefika mwisho hana vision kwamba kuna siku kipato chake kitakuwa kikubwa zaidi ya leo inshort amedumaa kimawazo?????
Na jee akioa mke mwenye kipato cha kawaida na baadaye bibie mambo yakawa safi kipato kikawa maradufu jamaa anakimbia tena duuuuuu-----------------!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Migodi mingine bhana!
Habari yako mkuu,dah nimefurahi kukuona humu!msimseme sana jamani........................mwenzenu kakimbiza ubavu wake bana .............kaona isiwe taabu!
Waambie wasikie!Jamaa noma...! Mke wako akiteuliwa kuwa Asha-Rose Migiro utamwacha? It's just a matter of logical thinking.
Wala hujakosea,Kimsingi sidhani kama jamaa anafikria straight, kwanini uombe salary slip ya mwenzio?????, Pili jamaa amefika mwisho hana vision kwamba kuna siku kipato chake kitakuwa kikubwa zaidi ya leo inshort amedumaa kimawazo?????
Na jee akioa mke mwenye kipato cha kawaida na baadaye bibie mambo yakawa safi kipato kikawa maradufu jamaa anakimbia tena duuuuuu-----------------!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Migodi mingine bhana!
Habari yako my Big Shem,hivi Canta una ruksa maalum kumesema mkasa wa binti hapa jamvini maana sitaki baadaye urudi na manundu usijekosa mume bure! ohoo😛oa
My sisy najua majukumu tu yalikubana au ulikuwa mitaa yako chit-chat!Mambo sister lisia? Hii thread imenipita sijui nilikuwa wapi.
Huyo mwanaume hajiamini nukta
Shikamoo babu,Orayt, hata mie naamini siyo wewe. Sasa waweza kutuambia hiyo salary slip inasoma mshahara wa huyo binti ni shingapi vile?