Hawa kikuu siwaelewi kwa kitu kimoja. Kwa nini soko limejaa tu nguo, urembo na vitu vidogo vidogo na hakuna vitu vikubwa kama zana za kilimo na viwanda? Je ni kwa sababu wanaona sisi hatuna uwezo wa kununua? Wanakwepa gharama za usafirishaji? Serikali inawabana au ni nini hasa?
Maana na sisi tungependa kupata vitu vya kufanyia uzalishaji ili kuinua uchumi wetu sio urembo tu. Kiukweli hata ukisachi kompyuta tu Kikuu haimo!