Jaribu moja kati ya hiz dawa kutumia isipo msaidia unatumia Dawa ingine kisha uje hapa unipe feedback.
Dawa ya kutibu Maradhi ya kutoka Damu Puani. Chukuwa maziwa uyachemshe hadi yamechemke vizuri na uyatie katika gilasi, kisha chukuwa yai bichi ulipasue na kulimimina ndani ya hayo maziwa. Koroga mchanganyiko huo wa maziwa na mayai na kuacha hadi yapoe. Kunywa yakishapoa. Tumia hivyo Asubuhi kabla ya kula kitu na usiku kila siku mpaka apone hayo maradhi inshallah atapona kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu .
Au tumia dawa hii pata siki kwa kiingereza inaitwa (Vinegar) kijiko kidogo changanya na maji ya wa mawaridi kwa kiingereza inaitwa (rose water) kijijko kidogo, mtilie matone matone kwenye tundu za pua yake hukatisha kutoka hiyo Damu.
Au tumia dawa hii jaribu kumnusisha huyo mgonjwa hiyo siki kwa kiingereza inaitwa (Vinegar) hiyo damu itakatika.
Au tumia dawa hii chukuwa mavi ya njiwa uyaponde, kisha uchanganye na siki kwa kiingereza inaitwa (Vinegar) ya zamani ,kisha mgonjwa awe ananusa kila mara damu ya kutoka puani itakatika inshallah jaribu Mwenyeezi Mungu atajaalia mwanao atapona inshallah.
Au Tafuta miba ya mnyama anaitwaye nungunungu kisha uuchome na kunusa puani moshi wake hutakaa uone tena.
Au tafuta majani ya mbaazi yafichike kisha mtie puani.