Msaada tafadhali: Ni kipimo gani kinatumika ili kujua kuwa mwanamke ana uwezo wa kuzaa?

iron woman

Senior Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
147
Reaction score
19
Samahani wandugu,

Naomba msaada; mwanamke anawezaje kujua kuwa ana uwezo wa kubeba mimba na kuzaa? Anatakiwa kupima kipimo gani ili kujua kizazi chake kiko vizuri na ana mayai?

Naomba kueleweshwa
Asanteni.
 
Anza na transvagina utrasound kucheki kizazi....
Blood test kucheki hormone levels....

Utaanzia hapo
 
iron woman, hii kitu ni process ndefu. Ila njia ya kwanza ni kichunguza mzunguko wa hedhi(menstruation cycle),kubadilika badilika kwa mzunguko au ile damu inayotoka ikiwa na mabonge makubwa hapo yawezakana kuna tatizo.

UPIMAJI HOSPITALI UTAHUSISHA VITU VINGI MFANO;
njia za uzazi unazotumia,surgical history, lifestyle,medication history nk.
Pia unaweza ukachunguzwa tezi ya thairoid na matiti.

Kipimo kikubwa kitakachotumika ni ULTRA SOUND.
utachunguzwa Ovarian fuctioning,kuona ufanyaji kazi wa homoni za uzazi na kupima damu ili kujua kiasi cha INHIBIN B, hasa kipindi cha ovulation.

Pia uchunguzi hufanywa kupitia kwenye VAGINA(UKE).
Huko huangalia yale majimaji/utelezi uliopo kama unaweza kuruhusu mbegu za kiume zipite bila tatizo,kipimo huitwa POST COITAL TEST(PCT). pia utachunguzwa bacteria wanaokuwepo huko.
Ultrasound itatumika kuangalia upana wa ukuta wa uterus kama unaruhusu mimba kujishikiza, hii hasa hufanyika katika kipindi cha uvulation (siku za hatari wengi wanaita hivyo).

NJIA NYINGINE NI;

HYSTEROSALPINGOGRAM (HSG)- hii ni x-ray ya mfuko wa uzazi na mirija ya falopia inayopitisha mayai.

HYSTEROSCOPY- hapa kifaa kinaitwa Hysteroscopy kinaingizwa kupitia kwenye cervix(ukeni) mpaka kwenye mfuko wa uzazi(uterus) na docta anaangalia kama kuna tatizo lolote humo.

LAPAROSCOPY:- laparoscopy ni kifaa chembamba sana kama sindano, unachomwa kinaingia mpaka ndani,kina kamera hivyo dokta ataweza kuangalia mirija ya falopia(fallopian tubes) na uterus kama vipo sawa.

NB; Si lazima vipimo vyotr hivyo vitumike. Unaweza kuishia kwenye ultra sound, hivyo vingine hutumika ikiwa kuna wasiwasi juu ya majibu ya ultrasound au kupata uhakika zaidi..
 
Last edited by a moderator:
Vipi gharama za huduma hii na zinapatikana hata vituo vya kawaida?
 
nashukuru sana ndugu nimekuelewa vizuri kabisa.
kilichobaki kufanyia kazi.
asante
 
Last edited by a moderator:
nakushauri nawewe upime pia maana unaweza mpima mke kumbe nawewe ni shida.

wengine wakipimwa wanaambiwa wako poa kumbe sperms ziko weak
 
Back
Top Bottom