Msaada tafadhali: ni wiki na nusu sasa sijapata choo

LAKI

Senior Member
Joined
Jun 12, 2013
Posts
100
Reaction score
37
Habari wana JF! Poleni na majukumu ya kila siku,

Naombeni msaada tafdhali, ni wiki na nusu sasa sijapata choo, tumbo haliumi ila nina wasiwasi maana hali imetokea gafla sijawahi kuptiliza hata siku moja pasipo kupata choo. Sijabadilisha mazingira wala mlo, asubuhi chai kama kwaida, mchana chakua na jioni mara nyingi nakula matunda na mbogamboga, maji nakunywa ya kutosha kama lita 3/4 kwa siku.

Sijui ni nini kimetokea kwa kweli.

Wenye kujua naombeni msaada tafadhali niweze kurudi katika hali yangu ya kawaida maana inansababishia maumivu ya kichwa na mwili kukosa nguvu.

Asanteni.

 

Embu jaribu siku moja ukishakula ukapumzika either jion au asubuhi piga zoezi hasa la kamba au kukimbia kwa dakika 20 au 30 alafu ulete feedback!!!
BTW pole sana mkuu... unaeza jaribu hiyo njia nliyokupa...
 

Mkuu kula sana Matunda!
Ukianza na madafu itakuwa poa! Lakini kuwa makini usije ukapumua hadharani, unaweza ukawapotezea watu hewa yao ya oxygen!
 
Kula parachichi mbili na ndizi tatu gogo lazima likigoma kama una wiki kimbia kituo cha afya
 
Kunywa maziwa mgando kahawa na ndizi utaharisha baada ya nusu saa tu.
 
Hahahahahahhahahahahahahashahahahahaàaaaaaaaaa.........
 
Mapapai husaidia sana kama unakosa choo, kitu kingine angalia na aina ya mlo unao kula, wali/vyakula vya ngano/nyama tupu huwenda vika sababisha constipation, so jaribu kuchanganya na mboga za majani kama mboga maboga (ni nzuri sana), kabichi na nyinginezo.

Piga mapapai utaona matokeo.
 
Hahahahaaa jf wadau mnafurahisha!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu (Constipation)...


UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida.

Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu.

Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?

Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa.

Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?

Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?

Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo:

Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda Choo. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi.

Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvuguvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu

yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil' muda mfupi kabla ya kwenda kulala.

Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi ya uvuguvugu kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na

kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate

myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu LAKI
 
Last edited by a moderator:

Asante sana Mizizi Mkavu, ngoja nianze leoleo kufuata ushauri wako. Ubarikiwe sana mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…