Msaada tafadhali;Nichukue hatua gani za kisheria?

Msaada tafadhali;Nichukue hatua gani za kisheria?

Stanboy

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2013
Posts
1,114
Reaction score
1,308
Nilimpa pesa mfanyakazi mmoja wa wizara fulani ili anisaidie kupata uhamisho kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Sasa ameshindwa kufanya hiyo kazi na hataki kurudisha pesa,
je naanzia wapi kisheria?
msaada tafadhali mnaojua sheria..
nawasilisha
 
Kwani hiyo pesa ulivyotoa ulipewa stakabadhi ya malipo? Kama sio hivyo imekula kwako ila kwa kuwa jamaa bado anatamaa na pesa basis mbembeleze mwambie umuongezee kiasi kingine cha Pesa ili akamilishe deal najua atakubali then kamchukulie Pesa za moto halafu umpe.hiyo inaitwa jino kwa jino .
 
umempa sh. Ngap? Na mimi nimpelekee anihamishe?
 
Kwani hiyo pesa ulivyotoa ulipewa stakabadhi ya malipo? Kama sio hivyo imekula kwako ila kwa kuwa jamaa bado anatamaa na pesa basis mbembeleze mwambie umuongezee kiasi kingine cha Pesa ili akamilishe deal najua atakubali then kamchukulie Pesa za moto halafu umpe.hiyo inaitwa jino kwa jino .

Nilimtumia kwa M-Pesa na message bado zipo,lakini pia message ninazochat naye zipo na zinajieleza wazi
 
Je hilo zoezi ni halali kuwa ulitakiwa ulipie hiyo pesa.

Naweza kusema siyo halali,
nilimuomba asaidie tu ndo akadai anataka japo chochote...
so sijui kama naweza kumbana kisheria ndo maana nikaomba msaada.
 
Naweza kusema siyo halali,
nilimuomba asaidie tu ndo akadai anataka japo chochote...
so sijui kama naweza kumbana kisheria ndo maana nikaomba msaada.

Hapo no way out coz we ulihitaji upendeleo so ukatoa rushwa na zoezi limebuma.sidhani kama kuna sheria inakulinda hapo.zaidi refer my 1st post
 
ww hiyo ni rushwa mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ndan jipeleke mwenyewe takukuru
 
habari,naomba na mimi nichangie hapo kidogo,katika sheria za mikataba(law of contract) kuna vitu batili ambavyo vikifanyika jicho la kisheria tangia mwanzo halivitambui na hivyo kukosa nguvu ya kisheria(void contract) au mikataba batili, kwakuwa ulichokifanya ni kutoa rushwa na ni kitendo batili hivyo huwezi kwenda kushtaki mahakamani kwakuwa sheria haitambui mkataba wa aina hiyo.pole ndugu.
 
Imekula kwako ndugu..hapo hakuna mkataba.....Note.all contracts are agreement,BT not all agreements are contract...
 
Umempa rushwa na hairuhusiwi kuhonga. Pole zako pesa imeenda unaona hata aibu kuitaja(hata kwa kiasi kingine cha karibu). Yaani utashindwa kesi.
 
Nilimpa pesa mfanyakazi mmoja wa wizara fulani ili anisaidie kupata uhamisho kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Sasa ameshindwa kufanya hiyo kazi na hataki kurudisha pesa,
je naanzia wapi kisheria?
msaada tafadhali mnaojua sheria..
nawasilisha

ulitoa rushwa hvy nawe unastahili ufunguliwe mashtaka
 
Back
Top Bottom