MSAADA TAFADHALI: Nini asili ya jina 'URENO'????

MSAADA TAFADHALI: Nini asili ya jina 'URENO'????

Minkya

Member
Joined
Nov 12, 2012
Posts
29
Reaction score
5
Habari wanajamvi!!

Nimekua nikifatilia sana maswala yahusuyo lugha yetu adhimu ya Kiswahili na mara nyingi huwa najaribu

kutafuta majibu kwanza mwenyewe kwa Misamiati mingi ya lugha, unakuta huwa tumekopa au yanaambatana

na visasili vichache vinavyokupatia maana halisi ya neno husika.

Nimekua kwenye mishughuliko fulan kipind cha ivi karibuni na nimebahatika kukutana na wanajamii wa mataifa

mengine hasa hasa ya Ulaya ivyo nimejikuta kila utaifa ninaokutana nao najiuliza Hivi kwa Kiswahili tunawaitaje

hawa halafu najaribu kuoanisha na utaifa wao....

mfano: French tunawaita Wafaransa sababu wanatokea France(Ufaransa) au

Spanish tunawaita Wahispania au waspanyola sababu wametokea Spain...nk

Utagundua herufi zinavojirudia kwenye majina wanavojulikana kimataifa(kiingereza) na Kiswahili

Sasa nikaja kwa jamaa ametokea portuguese, awa tunawaita WARENO au nchi yao tunaiita URENO...kwa nn??

Kiswahili tulilitoa wapi hilo jina Ureno....nn kisa??

Najua kuna wataalamu wa lugha yetu umu tafadhali naombeni msaada wenu!!!
 
Back
Top Bottom