Msaada tafadhali. Uhakika juu ya hili

Analyse

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
17,637
Reaction score
47,413
Nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu, hivi unauhakika gani rangi zote huwa tunaziona sawa?

Namaanisha mfano unaposema rangi ya njano, una uhakika gani kuwa mimi naiona kama unavyoiona wewe, au tunaongozwa tu na majina ambayo yameshawekwa?

Rangi kama udhurungi, hiyo ndio huwa naisikia tu, au pengine kwangu inajina jingine.

Kwanza jina udhurungi lilitokana na nini au lilitoka wapi?
 
Ukweli una parameters.mfano mtoto mdogo ukimpa 2000 ataiona kubwa ila mtu mzima ataiona Ni ya kawaida
 
Shule huwa wanafundisha kutaja majina ya Rangi
 
Rangi usipoiona sawa Huitwa COLOR BLINDNESS.. watu wapo wenye Disorder hiyo.. mfano. kijani anaiona nyekundu au nyekundu anaiona ni Kijani.
 

Uhakika juu ya ili [emoji777]
Uhakika juu ya hili [emoji818]

Udhurungi [emoji777]
Hudhurungi [emoji818]

Swali lako ni gumu sana kwa sababu linagusa dhana nzima ya nini ni uhalisi wa kitu tunachokiona? Nitajuaje kama meza ninayoiona kweli ni meza hiyo hiyo unayoiona? Uhalisia wa kitu ni nini? Je, nyekundu yangu ni nyekundu yako? Vipi kama nina colour blindness?...aaargh !!!
 
Kwa kesi ya vitu, hapo ni rahisi maana unaweza ukaelezea muonekano. Ila rangi unamwambiaje mtu jinsi rangi ilivyo

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Una uhakika gani hiyo wanayoiita nyekundu, kwamba mimi na ww tunaiona sawa?
Wachukue vitambaa 7 vyenye rangi yofauti, na tukaambiwa kujaza majina ya Rangi hizo.
Almost kama mtu anajua majina ya Rangi hawezi kukosea, majibu lazima yafanane.

Na tunaona sawa ndio maana utasikia mala blue mkozo na blue mpauko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…