mwanajamnvi, kama ni m2 binafsi mnatakiwa kuwa na makubaliano ya malipo, kama ni serikali pia unatakiwa ulipwe lakini sheria haijaweka kiwango maalum cha kumlipa mtu unayemwamisha lakini inataka mtu huyo alipwe kwa thamani ya wakati huo anapohamishwa. kwa hiyo kama ni sasa hivi unatakiwa kulipwa kwa thaman ya sasa hivi. mthamini atatakiwa aje na athamini maeneo hayo kwa thamani ya sasa, au kipindi hicho mnachoamishwa.
Kuhusu vigezo, hakuna vigezo maluum, inategemea na malengo ya eneo hilo, kwamba nini kinatakiwa kifanyike hapo, na hivyo kupitia sababu hizo mtatakiwa kuhama kwa makubaliano ya kulipwa kwa kuamishwa katika makazi yenu.