Msaada tafadhali

NZURI PESA

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2011
Posts
5,958
Reaction score
2,954
Kwa wana jf wenye ufahamu wa tatizo hili naomba ushauri wenu.
Kuna mtoto wa umri wa miaka 10,ana tatizo la ADENOIDS.Amekwisha wahi kufanyiwa upasuaji takribani mara 5 kwa kipindi cha miaka 5 lakini tatizo lake halijakwishaNimempeleka.Klinik naambiwa upasuaji tena!.Nini TIBA YA KUDUMU YA TATIZO HILI?Nawasilisha
 
Adenoids (au koromeo kifuko,) ni wingi wa nyama ya limfu iliyo nyuma ya matundu ya pua, juu ya koo na huingia ndani ya koo.
Kwa kawaida, kwa watoto hufanya maboma laini katika ukuta na juu nyuma ya koo, juu kidogo tu na nyuma kilimi.
Pia tofauti na aina nyingine kifuko kwa kukosa crypts. adenoids mara nyingi kuondolewa pamoja na tonsils. Hii inaweza kusababisha koo mazito sana kwa wiki moja na pumzi badala baya. Watu wengi adenoids ni hata katika matumizi baada ya mwaka wa tatu wa mtu [onesha uthibitisho], lakini kama kusababisha matatizo ya lazima kuondolewa [onesha uthibitisho] au wanaweza vinginevyo kuogopa.
Adenoid zinapokuwa kubwa husababisha mtoto kushindwa pumua , hivyo hutumia mdomo kupumua.
Mara nyingi watoto wenye ugonjwa huu pia sura zao hubadilika. uso huwa mrefu na mwembamba, mifupa ya chini ya macho ni mifupi, pua ao huwa ndefu. kaa (palate) juu ya mdomoni huwa nyembamba na ya kupinda kama nanga.
Upasuaji wa kuondolewa adenoids ni utaratibu uitwao adenoidectomy.
Adenoids huondolewa pale tu zipatapo maradhi na kusababisha mtoto kuwa na kamasi nyingi au kushindwa pua kabisa. Uchunguzi umeonyesha kuwa zaidi ya 20% adenoid hukuwa tena hata baada ya kuwa zimeondolewa.
kuna njia nyingi za upasuaji ili kuziondoa, kama vile laser, currets n.k. hivyo inakubidi ndugu umpeleke mtoto zikaondolewe tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…