Kwahiyo kinaitwa pia Kiswahili?
Na kama ni hivyo,vipo Viswahili vya aina ngapi wakuu?
Aina za uzungumzaji wa Kiswahili kunajulikana kama
lahaja. Wakati wa ukoloni wa Uingereza kilichaguliwa kutumia Kiswahili cha Unguja (
kiunguja) kuwa Kiswahili rasmi katika Tanganyika, Kenya na Zanzibar. Waingereza walikitumia pia kama lugha ya polisi na jeshi uko Uganda.
Hivi leo lahaja zilizo orozeshwa rasmi ni hizi zifuatazo:
*
Kiunguja: kisiwani Unguja (Tanzania) - kimekuwa msingi wa Kiswahili cha Kisasa.
*
Kimrima: eneo la Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji na Mafia kisiwani (Tanzania)
*
Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)
*
Kipemba: kisiwani Pemba (Tanzania)
*
Kimvita: eneo la "Mvita" au Mombasa (Kenya). Zamani ilikuwa lahaja kubwa ya pili pamoja na Kiunguja.
*
Kiamu: eneo la Lamu (Kenya)
*
Kingwana: Kiswahili cha Kongo
*
Shikomor: Kiswahili cha Komoro
*
Shimaore: Shikomor cha Mayotte (Mahore)
*
Shindzuani: Shikomor cha Anjouan (Komoro)
*
Shingadzija: Shikomor cha Komoro Kuu
*
Kimwani: Kaskazini ya Msumbiji na visiwa vya Kerimba
*
Chimwiini: eneo la Barawa, kusini ya Somalia
*
Sheng: Kiswahili cha mtaani Nairobi (Kenya) chenye maneno mengi ya asili ya Kiingereza, Gikuyu na lugha zingine za Kenya