Wadau wa elimu hebu tunaomba kumshauri ndugu yetu aliyehitimu kidato cha 6 na sasa hivi tupo naye jkt,
nisiende mbali coz amenituma niwafikishie kwenu na mumshauri yaliyomema,
kiujumla matokeo yake ya kidato cha sita hayakuwa mazuri alisoma mchepuo wa sayansi PCM
Na matokeo yake yalikuwa DEE,
kwenye matokeo yake
anasema walimwandikia 0 ya 17,
katika kutafuta nafasi ya diploma amepata nafasi kwakuunganishwa katika chuo flani,
swala linaanzia hapa hicho chuo wanataka matokeo ya kidato cha 6,
swali linakuja je!
Anaweza kupata cheti cha form 6 kwa matokeo hayo au afanyaje.?