Neno ‘awe' inamaanisha ‘uchaji'. Wakati wa nyuma watu hawalikutumia ‘awsome' sana kama walivyolitumia siku hizi; kwa ujumla walilitumia neno ‘awsome' kuhusu Mungu au kitu fulani ambacho kinasababisha uchaji moyoni mwako. Lakini siku hizi watu (hasa vijana) wanalitumia neno hili sana kuhusu jambo lo lote na kwa ujumla maana yake ni sawa na ‘ya ajabu'. Basi, siku hizi ‘awesome' hulinganisha na maneno ‘amazing'; ‘incredible', ‘wonderful'. Kwa hiyo, tukitafsiri neno hili kwa maana ya siku hizi, tunapata:
awesome = -a ajabu
I am awesome = Mimi ni wa ajabu! (Kwa keli?)
My God is awesome = Mungu wangu ni wa ajabu.
Neno hili limepoteza maana ya uzito ambayo lilikuwa nayo siku za nyuma. Kwa mfano:
‘Cristiano Ronaldo is awesome. He's the best player in the world!'
Miaka 40 iliyopita sentensi kama hiyo usingalisikia. Siku hizi ni kwa kawaida kwa jambo lo lote hasa miongoni mwa vijana. Aidha, wanatumia neno hili katika nyimbo ya kikristo.