Msaada: Tafsiri ya neno MASABULI.

DASA

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
1,031
Reaction score
302
Habari zenu members, Jamani naomba mtu anisaidie tafsiri ya hili neno MASABULI, linaonekana ni neno maarufu sana kwenye uwanja huu. huwa ninaposoma comments za watu hasa kama mtu hajaridhika au kufurahia hoja ya mtu anaishia kureply kwa kutumia hili neno mfano "Unfikiria kwa a kutumia masabuli nini" au "Acha kutumia masabuli". sasa Masabuli ni nini jamani!. nisaidieni labda ugeni wangu humu unanifanya nisielewe hili neno. Natanguliza shukurani.
 
Mleta mada nakushukuru sana hauko peke yako hata mimi hilo neno limenitatiza sana, i hope tutapata majibu humu.
 
Gazeti la Tanzania Daima trh 6 August 2011.
 
Neno hilo linatumika kuonyesha ufinyu wa kufikiri na kwa sababu kauli hiyo ilitolewa na Dr. Masaburi katika sakata la UDA akiwapasha wabunge hawana akili na kufikia kuwafananisha kuwa wanafikiria kwa kutumia makalio! Hivyo hapa JF linaweza kutumika kama tusi, peleka masaburi yako yaani peleka makalio yako au unafikiri kwa kutumia masaburi wewe. Yote kwa yote neno masaburi siyo zuri kwa minajili ya lugha inavyobadilika na jinsi linavyotumika.
 
kweli utajua tu ambao hawasomi jukwaa la siasa.
 
Nashukuru sana mkuu kwa ufafanuzi wako mzuri.
 

Nashukuru sana mkuu kwa ufafanuzi wako mzuri.
 
Saburi = Kalio,
Masaburi = ........!!!!
 
naamini hadi sasa mtakuwa mmepata tafsiri sahihi juu ya neno hilo ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…