tzhumoally
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 412
- 156
Wakuu nipo Sumbawanga kwa muda huu, juzi nimetoka nilimpeleka mdogo wangu shule (amepangiwa Mambwe sec school) ila kwa kweli mazingira hayaridhishi kabisa, hakuna walimu na umeme pia hakuna, sasa nimeambiwa hapa Sumbawanga kuna shule inaitwa Kantalamba, nataka nijaribu kumfanyia mpango wa uhamisho kama ikiwezekana, naomba ushauri nianzie wapi maana sina uzoefu ya haya mambo, nataka nifanye hio mipango kabla sijaondoka huku Sumbawanga.