Msaada tarehe ya kupata mimba

Kwani mzunguko huendana na tarehe za kwa kalenda maana apo naona 31 wakati on average wengi wako kwa 28 days
mi zakwangu ni kuanzia 29 hadi 31 kwa kawaida sijashuka kwenye 28
 
mh hapo sasa maana unanichanganya samahani biology F nifafanuliemaana daaaa
 
Mi sijui hayo mambo kiivyo, lakini naona hii yako ni mpya, unaweza ukamfanya mtu akapata matokeo asiyotarajia kabisa, na akachanganyikiwa.


Tatizo la mchoro ni zile siku tatu zinazooneshwa kuwezesha mimba siku chache tu baada ya hedhi. Pia utabiri wa mtoto wa Kiume haujakaa sawa. Ile sehemu ya pili ni sahihi kwa uwezekano wa mimba lakini kutabiria mtoto wa kiume kwa siku ile ya kwanza pia si sahihi. Mtoto wa kiume haji kwa jab siku ya kwanza. Kuna sababu tofauti na hiyo nina hakika.



Jaribu hii itakusaidia kwa mapenzi ya Mungu

View attachment 87510
 

Je kusafiri hakuathiri ovulation?
 
Je kusafiri hakuathiri ovulation?

Sidhani kama tuite kusafiri moja kwa moja, ila ninavyojua kuwa kubadilisha mazingira kwa ghafla kunaweza kuathiri mzunguko wa "Menstrual Circle".
Lakini sio mara zote hali hii huwakumba kina mama wote.
 
Kiufupi MadamG nina maanisha kwamba, kuna sababu nyingi sana za kutokubeba mimba.zingine ziko upande wa mwanaume, na zingine ziko upande wa mwanamke, na zingine zinawahusu wote kwa pamoja.Kupata damu ya hedhi sio kigezo pekee kinachoweza kumfanya mtu abebe mimba.Je kuna kipimo ulifanyiwa kuthibitisha kwamba yai linatoka kila mwezi(ovulation), je mirija ya uzazi(fallopian tube) iko sawa?, na je mwenzako anatoa mbegu za kutosha, na je mnafanya tendo kwa wakati.Wataalamu wanasema wakati mwingine mnaweza mkapimwa mkakutwa mko sawa, tatizo lenu likawa ni Timing of intercourse.Hapa watu wengi wamechangia zaidi kuhusu timing of intercourse bila kukuuliza mambo mengine. '
Tunavyojua ni kwamba katika kundi la wanandoa 1000, wenye afya nzuri, wanaokutana kimwili kwa wastani wa angalau mara 3 kwa wiki, baada ya miezi 6 asilimia 80% watakuwa wamebeba ujauzito, na mwisho wa mwaka huo ni 95% ya jumla hiyo watakuwa wamepata ujauzito.Na hii ni kwa wale wanawake wenye umri wa chini ya miaka 35. kuanzia miaka zaidi ya 35, utengenezaji wa mayai ya kike unaanza kupungua kwa kiasi kikubwa.na chance ya kupata ujauzito inapungua.sijui wewe una miaka mingapi? je umeolewa au mnakutana na rafiki kwa siku ambazo mnahisi ndiyo za ovulation?how frequent is your intercourse? kuna maswali mengi yanahitaji majibu hapa.
mh hapo sasa maana unanichanganya samahani biology F nifafanuliemaana daaaa
 
Last edited by a moderator:
Sidhani kama tuite kusafiri moja kwa moja, ila ninavyojua kuwa kubadilisha mazingira kwa ghafla kunaweza kuathiri mzunguko wa "Menstrual Circle".
Lakini sio mara zote hali hii huwakumba kina mama wote.

Unaweza kukuta kuwa umesafiri/umebadili mazingira lakini siku za period hazijabadilika.Sasa je inaweza kuathiri ovulation?
 
Unaweza kukuta kuwa umesafiri/umebadili mazingira lakini siku za period hazijabadilika.Sasa je inaweza kuathiri ovulation?

"Nina mfano hai mmoja ambao ulimtokea mke wa rafiki na kupelekea kupata mimba pasipo kujua.
Mwana mama huyo miaka yote amekuwa akiishi Dar es Salaam, sasa kuna wakati alisafiri kwenda Iringa kikazi.
Jumla ya siku zake za mzunguko huwa ni siku 29, sasa siku aliyorudi Dar es Salaam ilikuwa ni siku yake ya mwisho ya Menstrual Circle yaani 29 ambayo kiasili mwanamke hawezi kushika mimba.
Kilichotokea kwa mwanamama yule siku hiyo alikutana faragha na mumewe, baada ya wiki 2 mwanamama akagundua ana mimba baada ya kuona siku zake zimesita kuja."


Nadhani kwa mfano hai huo unaweza kuona kwamba hata Ovulation huweza kubadilika pia.
 

Nimeku-PM tafadhali.
 
nina miaka 30, nimeolewa ingawaje mara nyingi nipo mikoani kikazi suala la kutafuta mtoto sijaanza mda mrefu ni kama mwezi uliopita sema niliuliza ili nisibaatishe pia kuusu kwenda hospitali bado sijaenda. hapa nina swali baada ya kumaliza blidi uwa vinatoka vitu kama vinanata nata nilipata kusikia kipindi hicho kuwa ni siku za hatari je unaweza ukapata izo dalili na usiweze kushika mimba?
 

Hakikisha unampa msosi mzuri mwenzio ili akojoe mbegu zenye ubora.
 

Hii fani ni bailoji ya form iv? Na uhakika dogo utapata PM kibao kwa kina mama ila chonde chonde usiingie majaribuni.
 
Hii fani ni bailoji ya form iv? Na uhakika dogo utapata PM kibao kwa kina mama ila chonde chonde usiingie majaribuni.

Mambo ya uzazi hayaihitaji elimu ya darasani tu, ndio maana miaka ya nyuma tulikuwa na Wakunga wa Jadi.
Hahah eti PM...Darling measkron naomba msaada wako kwenye kuwasaidia hawa kina mama.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kawaida mwanaume ana XY wakati mwanamke ana XX. XY ni mbegu zilizopo kwa mwanaume wakati XX ni mayai yaliyopo kwa mwanamke.Mbegu X iliyoko kwa mwanaume ina speed zaidi ya Y. X iliyoko kwa mwanaume huishi saa 24 na hufa wakati Y speed yake ni taratibu na hudumu kwa masaa 72.X husababisha mtoto wa kike wakati Y husababisha mtoto wa kiume.Unapokutana na mwanamke siku ya sita tangu amalize hedhi huweza kusababisha mtoto wa kuime kwasababu yai XX la mwanamke linakuwa halifika nyumba ya uzazi. Wakati huo XY zinapokuwa kwenye nyumba ya uzazi zitadumu saa 24 mbegu X ya mwanaume inakufa na kubaki Y ikisubiri yai X toka kwa mwanamke kufika nyumba ya uzazi. Hivyo maana yangu katika kuweka "mtoto wa kiume au mtoto wa kike, ilikuwa ni katika mtazamo huo" Maana halisi ni kuwa mwanaume anatakiwa kulala na mwanamke siku ya sita halafu aache asubiri matokeo ili aweze kupata mtoto wa kiume kwani alifanya tena na siku ya saba atakuwa ameweka mbegu X itakayo dumu siku nzima nyingine wakati ile X ya jana yake imeshakufa na kubaki Y ikiisubiri XX ya mwanamke kuungana kupata Baby boy.
 

mmh! ok...maybe.
ila pia nilisikia kuwa badala ya hiyo kazi yooote ya kuvizia kijiyai tumboni ukitaka mtoto wa kiume unaenda tu msitu wa Kisarawe, Pwani, nasikia kuna kimzizi kule unatafuna, halaf kesho yake mnanalii basi....mnapata mnachotaka.
 

Nmesoma comment yako, ulichoandika ni sahihi 50% nikiwa kama mwalim, hizo 50% ulizoshindwa ni kwenye spidi na life time of X and Y-sperms.

Y-sperm are the one which are faster than X-sperm and they die quickly (48 hours),

X-sperm, are slower in speed but they have long life span (72 hours).

Viti vingine viko sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…