Habarini za asubuhi wakuu,
Mimi nasumbuliwa na Macho. Nilianza kuvaa miwani tangu 2008. Na huwa kila mwaka au miaka 2, napima na kupewa miwani mingine. Sasa mwaka huu, macho yakanisumbua, yanashituka nikiona mwanga, misuli inayozunguka macho inauma, hadi kichwa cha mbele na pembeni kuelekea masikio.
Nimeenda kupima mwezi wa 8 mwaka huu, wakanipa miwani mingine na dawa ya matone. Pamoja na hivi bado macho yanasumbua sanaa. Yanapoa siku 1 au 2, hali inarudi ileile. Kazi zangu natumia Computer muda mwingi kwa kutumia miwani hihii, kwa miaka 20 sasa.
Naombeni ushauri wenu wakuu.