Msaada tatizo la ngozi usoni

JIGOKU IKAYA

Member
Joined
Apr 29, 2017
Posts
38
Reaction score
46
Habari zenu wanajamvi? naomba ushauri na matibabu nina tatizo la ngozi ambalo limenisumbua kwa muda mrefu karibu miaka kumi sasa linavyokuwa lipo juu kidogo kwenye jicho la kushoto uanza kwa ngozi kukauka Kuwasha unapokuna hutoa magamba.
Baadae hutoka vipele ambavyo huwa na majimaji, katika hali hii vipele huungana na kuwa kidonda.

Kidonda huuma kufunika jicho lote, nafuu yake kwa muda wote huo nimetafuta tiba sehemu mbalimbali bila mafanikio lakini kuna dawa ambayo hunisaidia sana angalau kwa mwezi/miezi kadhaa dawa hiyo inaitwa BETASOL.

Kuja hapa jukwaani ni kupata tiba au ushauri maana nimesumbuliwa muda mrefu sana.
Je kuendelea kutumia betasol kuna madhara?
Nawasilisha.
 
Nenda kawaone madaktari wa ngozi
We unategemea miaka yote kumi hajawahi kwenda hospitali???
Hapa kaja kuomba wenye experience za magonjwa kama hayo wamsaidie, or tiba mbadala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…