Msaada: Tiba ya nyama za puani

Song of Solomon

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
2,752
Reaction score
5,609
Habari za asubuhi ninaomba msaada kwa mwenye kujua tiba mbadala ya NYAMA ZA PUA nje ya kufanyiwa operation ninasumbuliwa na tatizo hili zaidi ya miaka 15 sasa hadi imefikia nimetatiwa mnoo naishi kwa kutumia dawa ili niweze kupumua nimechoka kwakweli mwenye uelewa wa tiba mbadala anisaidie[emoji120]
 
Niliwahi kulazwa mara mbili kwa ajili ya kufanyiwa operation ikashindikana sababu ya pressure kupanda nikiwa theater
 
Asante..

Haupo peke yako mkuu wimbo ulio Bora. Tupo wengi.

Cha muhimu ni kuikubali hali na kuepuka vichochezi.

Mimi nina hili tatizo, mwaka wa 13 sasa na nimeishi Kwa dawa hadi nikachoka.

Nimejikita kwenye maombi sasa. Angalau hali imepungua, yaani sasa hivi nadeal na maombi tu!

Nitaleta feedback nikifanikiwa.
 
Same scenario nilikuwa nayo. Yaani ukiingia theater pressure iko high muda wote. Wakataka wanipatie dawa za pressure ili ishuke ndio wanifanyie. Akatokea dkt mmoja akapinga shauri hilo.
Nilikaa theater almost two hrs nikiongeleshwa ongeleshwa ili pressure ishuke (kumbuka hapo nishalipa mkwanja mrefu juu ya hilo)
Basi nikafanyiwa hivyo hivyo kuja kuzinduka nina mabandeji puani niko wodini.
Nashukuru Mungu nahema fresh mda mwingine najihisi kama pua ziko wazi.
 
Tupo wengi...mi ni mwaka sasa nasumbuka
 
Aisee mimi scenario yako iko kama mimi mpaka naanza kuogopa kuingia theater tena maana Dr aliniambia ili operation ifanyike lazima pressure iwe kawaida sababu damu haitakiwi kutoka sehemu ya pua maana madaktari watashidwa kuziona
 
Ni operation Tu.
Fanya na Kila kitu kitakaa sawa with in few days utakuwa poa na utashangaa ulichelewa Nini.
All the best
 
Ni operation Tu.
Fanya na Kila kitu kitakaa sawa with in few days utakuwa poa na utashangaa ulichelewa Nini.
All the best
Shida ni pressure ndg yangu natamani sana kufanya operation naogopa mnoo hii issue
 
hiii Mada imeisha hivi hivi bila suluhisho...hii inaonesha hili tatizo halina tiba ni kukomaa nalo tu had utwaliwe
 
hiii Mada imeisha hivi hivi bila suluhisho...hii inaonesha hili tatizo halina tiba ni kukomaa nalo tu had utwaliwe
Nikweli Mkuu sijapata suluhisho lolote namimi naaminj hapa jamii forum ndy mwarobaini wa matatizo lukuki[emoji11]
 
Ulifanya operation hospitali gani? pia vipi kuhusu presha saizi iko poa?
 
Nyama za puani zinatibika bila operation,ingawa pia kuna wale ambao wanafeli kupona na wengine wanapona kabisa.Hivi ni viotea kama ambavyo mtu anaota nyama sehemu za haja kubwa au sehemu za kike pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…