Msaada toyota ractis 1nz engine..

mabwiku

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
447
Reaction score
390
Habarini wakuu,kama nilivyoandika juu hapo ninayo Ractis ina engine ya 1NZ anatumia wife,sasa imeanza tatizo ambalo naitaji ufumbuzi,ukiendesha kama km 150 hivi kuna muda inapunguza speed then inaenda ikikaribia kusimama inazima then inabaki switch on, ukiwasha haipokei moto mpaka ipoe then ukiwasha inakubali,nimechunguza linapotokea tatizo hilo kucheki kma inachemsha lakini haichemshi,taa ya check engene kuashiria tatizo haiwaki ila inawaka kawaida.
 
Unatumia oil gani kwenye engine? na je system ya maji inakwenda sawa?
 
Hapo matatizo yanaweza kuwa kama sio mafuta au umeme/crank shaft sensor.

Mafuta kuna mawili aither fuel filter au pump kama filter chafu inamaana gari itatembe kwa mda fulani uchafu unastick kwenye filter mpaka mda flani inaziba kabisa au kama ni pamp basi inatembea kwa mda then iki heat ina kata..

Crank shaft sensor ndio haswa huo huwa unakuwa ugonjwa wake na ndio dalili yake kubwa huanza hivyo lkn kadri utakavyokuwa unaendelea kuitumia mda wakuzima utapungua na maanisha kama ulikuwa ukitembea km10 ndio inazima basi itaanza kuzima baada ya kila km5 ukiendelea kutumia itashuka zaidi..

Sasa kama kujua kama ni hiyo sensor kama huna ya kujalibia tafuta maji ya baridi kutoka kwenye friji yabaridi kweli kweli tembeza gari ikizima fungua sensor mwagia maji ya baridi funga washa gari itawaka..hapo unakuwa umehakiki kwamba sensor ndio shida..au kama vipi ikizima wewe force kuendelea kuwasha then chukua mashine pima itakuonyesha shida.

Au kama ikigoma ww chomoa sapesa coil then angalia kama inatupa spark au laa .

Au kama upo bongo njoo mwenge mm nitakusaidia kuku kagulia kujua shida ni nn then utachagua nikulekebishie au ukajipange ukalekebishe kwa fundi wako ..na kama mm nikulekebishie basi ww utagaramikia spare tuu.

Na kukutambulia shida yako ni nn kwenye gari yako nitakufanyia free kabisaa
 
asante mkuu kwa moyo wako huu,natamani sana ningekua dar ila nipo bukoba nitafanya ulivyoelekeza then nitaleta mlejesho
 
Mkuu ulifanikisha kumaliza tatizo lako?
 
M
Mkuu hilo tatizo ni starter imekufa, so ukiwa unaendesha inapata moto, ukizima gari haiwezi kuwaka mpaka ipoe. Hilo tatizo limenisumbua sana nimebadirisha starter last month sasa iko vzr tu
 
Gereji yako iko wapi mkuu tukuletee wateja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…