Msaada:Trafic case inaweza geuzwa kuwa case ya Madai!

Msaada:Trafic case inaweza geuzwa kuwa case ya Madai!

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
3,930
Reaction score
4,912
Wakuu nawasabahi!!

naomba kupewa ufahamu wa haya mambo ambayo mara nyingi tumekuwa tukinyanyaswa na Trafic Police bila hata kujua sheria zao.
Hivi unapokuwa charged na trafic case na ukatozwa faini baada ya hukumu trafic case hiyo inaweza kuwa case ya madai?na ni kwa tukio gani ambalo linawezapelekea trafic case kuwa case ya madai.
nashukuru wakuu.
 
naona sijakufahamu hapo. Unaweza kubainisha kesi gani hizo. Nipe mlolongo mzima ili niweze kukubainishia kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

Unaposema Traffic case hizi zina fall na unaeza kuzipata katika Police General Order (PGO).
naomba maelezo yako tafadhali
 
naona sijakufahamu hapo. Unaweza kubainisha kesi gani hizo. Nipe mlolongo mzima ili niweze kukubainishia kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

Unaposema Traffic case hizi zina fall na unaeza kuzipata katika Police General Order (PGO).
naomba maelezo yako tafadhali
Mfano ni kama vile wewe umemcrash mtu na yeye mnaenda mahakami unakutwa na kosa kuwa ulkuwa mzembe katika uendeshaji wako uakahukumia kutoa faini baada ya hapo mnaambiwa kuwa kila mmoja afuate utaratibu wa insurance yake.

Je upande mwingine unaweza kuktaa rufa na kufungua kesi ya madai yaani upande ule ulioshinda?
 
Kasi ya madai inajitegemea, haihusiki moja kwa moja na kesi ya kuvunja sheria.

Madai ni wewe Vs. huyu anayetaka fidia. Kesi ya kuvunja sheria ni wewe Vs. serikali.

So yes anaweza akakufungulia kesi ya madai.
 
Kesi ya traffic ni kesi ambayo Jamhuri hufungua dhidi ya mwenye chombo cha usafiri kwa kusababisha ajali yaletayo kifo, maunivu au uharibifu wa mali za mtu mwingine ambaye au yumo ndani ya chombo hicho au hata aliye nje ya chombo hicho. Mlalamikaji katika kesi hiyo ni Jamhuri na mshtakiwa huwa yule aliyesababisha madhara.

Kesi hizo husikilizwa kama kesi nyingine zozote za jinai na matokeo mwisho wake ni faini, kufungwa au kufungiwa leseni kutokana na ukubwa wa kosa lenyewe na haki ya kukata rufaa kwa adhabu zote hizo hapo juu ni mahakama kuu.

Kutiwa hatiani kwa kosa hilo haina maana kuwa muathirika hana haki ya kufungua kesi ya madai kudai fidia kutokana na maumivu, madhara na hasara inayotokana na ajali hiyo. Mara nyingi hukumu ya kesi ya jinai hutumika kama ushahidi wa uzembe kwa dereva aliyesababisha ajali.

hakuna unyanyasaji hapo huo ndo utaratibu.
 
Back
Top Bottom