Kesi ya traffic ni kesi ambayo Jamhuri hufungua dhidi ya mwenye chombo cha usafiri kwa kusababisha ajali yaletayo kifo, maunivu au uharibifu wa mali za mtu mwingine ambaye au yumo ndani ya chombo hicho au hata aliye nje ya chombo hicho. Mlalamikaji katika kesi hiyo ni Jamhuri na mshtakiwa huwa yule aliyesababisha madhara.
Kesi hizo husikilizwa kama kesi nyingine zozote za jinai na matokeo mwisho wake ni faini, kufungwa au kufungiwa leseni kutokana na ukubwa wa kosa lenyewe na haki ya kukata rufaa kwa adhabu zote hizo hapo juu ni mahakama kuu.
Kutiwa hatiani kwa kosa hilo haina maana kuwa muathirika hana haki ya kufungua kesi ya madai kudai fidia kutokana na maumivu, madhara na hasara inayotokana na ajali hiyo. Mara nyingi hukumu ya kesi ya jinai hutumika kama ushahidi wa uzembe kwa dereva aliyesababisha ajali.
hakuna unyanyasaji hapo huo ndo utaratibu.