Msaada:Tumbo kujaa gesi,kujamba kwa sauti kubwa,mdomo kuwa mchungu na kutoa jasho lenye harufu ya ho

Msaada:Tumbo kujaa gesi,kujamba kwa sauti kubwa,mdomo kuwa mchungu na kutoa jasho lenye harufu ya ho

Master Legendary

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
576
Reaction score
876
Wenye uelewa naomba msaada itakuwa ni ugonjwa gani?

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Tumbo kujaa gesi ni mojawapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume,,
 
yaani mwanaume unaja.mba....utavalishwa sketi muda si mrefu.
 
Wewe utakuwa umekula vya watu wewe, alafu hukuonesha shukrani... Dawa yake nenda kaseme asante...
 
Wenye uelewa naomba msaada itakuwa ni ugonjwa gani?

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Pole sana inaonyesha wewe hupati hata haja kubwa kwa wepesi? inaonyesha unaweza kukaa siku zaidi ya 3 huwezi kwenda choo kikubwa? una matatizo ya kutopata haja kubwa kwa urahisi hayo ndio matatizo yako makubwa ndio yanayo kusababisha upatwe pia na gesi kujamba kwa sauti kubwa na kutokawa jasho lenye harufu. Pendelea kula sana mboga za majani ,matunda na pia uwe unakunywa sana Maji ya uvuguvugu matatizo yako yatakwisha.

GESI TUMBONI (COLIC): Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo.

TIBA: Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni.
 
Wenye uelewa naomba msaada itakuwa ni ugonjwa gani?

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Mkuu,

Nadhani una ugonjwa unaosababishwa na bakteria wa helico. Nenda hospitali watachukua vipimo vya damu na pia unahitajika kupeleka haja kubwa kwa uchunguzi zaidi. Kama magonjwa mengine yote yanayosababishwa na bacteria ugonjwa huo unatibika vizuri tu na antibiotics. Ni ugonjwa uliogundulika siku nyingi kwenye nchi za wenzetu lakini kwetu haujulikani sana, ingawa kwa mawazo yangu ni ugonjwa unaoathiri watu wengi sana bila wenyewe kufahamu. Kwa kawaida mtu anaweza kuwa nao kwa muda mrefu bila kupata madhara makubwa na ndiyo sababu haufanyiwi uchunguzi na kupatiwa tiba.

Helicobacter pylori - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Kama yaliyosemwa hapo juu zingatia nenda muone daktari ujue unaumwa nini halafu ndio utafute dawa umeenda na wamesema ni nini
 
Back
Top Bottom