Wakuu, nimekuwa nikishawishiwa na baadhi ya rafiki zangu kujiunga na biashara ama shughuri zinazohusiana na kampuni ya telexfree. Nimekuwa nikipewa maelezo yanayo onyesha dhahiri mafanikio makubwa ya kipato baada ya kujiunga na kaampuni hiyo yenye shughuri kupitia mtandao wa internet. Mimi ni mtu mwenye kipato cha kawaida kabisa kwa vipato vyetu watanzania. Ninaomba ufafanuzi thabiti kwa anayejua zaidi ili nami nifanye maamuzi sahihi ama kujiunga ama kutojiunga kabisa. Naombeni mawazo yenu ma GREAT THINKERS.