matapeli hao, hio laki nane yako bora ufungue kibanda cha chipsi, utazungusha hela ndefu afu utaishia kupata comision elfu ishirini, hapo provided hujakosea kuuza, maana ukikosea kuuza luku ka ni wa elfu tano ukaweka elf hamsini imekula kwako hela hairudi, ka ndo umekosea mita namba ndo uhesabu loss, sikushauri hio biashara, tafta biashara nyingine ya kuinvest, hapo mtandao bdo haijasumbua bado, sio ka nakukatisha tamaa ila ukinunua utakuja ikumbuka hii post, utaishia kuifungia mashine kwenye kabati na kuwaza hela yako uliopoteza, unaweza ukanunua mwezi mmoja ikaharibika utaanza kuambiwa kuitengeneza laki mbili na sabini,charger zao ukikaa nayo miezi miwili unashukuru,ikiharibika unaambiwa elfu 30, yan utajikuta ata umetumia milioni mbili ukijumlisha kuinunua,kuitengeneza na loss za miezi miwil ya kwanza alafu comission ya miezi yote miwili labda ndio elfu 50,alafu kampun inakula sawasawa naww, yan ww ukipata elfu 50 ujue yenyewe imeweka kibindon elfu hamsini au zaidi, ni biashara ya kinyonyaji sana, serikali ingeingilia kati ugawaji wa faida kati ya kampuni nawajasiriamali maana wananyonywa, apo bado hujagombana na wateja mpka ukakosa usingizi, unalipia leseni au umeme afu risiti haitoki alafu hela ushakatwa, ukirudisha hela ujue imekula kwako, usipomrudishia mteja hela afu risiti humpi ka mtu ana akil mbovu afu ana haraka anataka kusafiri afu wewe unamwambia risiti haitoki, alafu ukiwapigi maxmalipo simu zinatumika au hazipatikani, unakuja kuwapata baada ya masaa mawili, yaani kati ya watu mia walionunua mashine za maxmalipo 96 wanajuta na wanaonea uchungu hela walioipoteza....nawasilishaWadau nataka kununua mashine ya MaxMalipo. Naomba yeyote mwenye information ya sehemu zinapopatikana na jinsi ya kuiunganisha na mtandao, tafadhali ani PM.
Natanguliza shukrani zangu.