Msaada tutani: Mwenye mkataba wa biashara ya Bodaboda

mrejesho wa kitu gani mkuu

Mrejesho wa jinsi biashara inavokwenda na changamoto zake. Huenda changamoto utakazokutana nazo zikamsaidia mtu mwingine anaeanza au anaefanya biashara hii
 
Mrejesho wa jinsi biashara inavokwenda na changamoto zake. Huenda changamoto utakazokutana nazo zikamsaidia mtu mwingine anaeanza au anaefanya biashara hii
Nifoadie na mm mkuu huo mkataba Pm
 
Mrejesho wa jinsi biashara inavokwenda na changamoto zake. Huenda changamoto utakazokutana nazo zikamsaidia mtu mwingine anaeanza au anaefanya biashara hii
vijana wengi wa bodaboda licence zao zikimalizika muda hawa renew hapo kuwa makini,hakikisha umelipa sumatra,bima,nenda kwa usalama,fire extinguisher na kadi vyote viwekwe kwenye pikipiki,hakikisha service inafanyika,tafuta dereva asiyekunywa wala kuvuta sigara na usimpe sharobara weka mkataba wa mwaka mmoja then dereva anabidhiwa pikipiki inakuwa yake hapo ataitunza
 
Fanya biashara mkuu achana na hao wanaokwambia ni biashara kichaa
 
Weka hiyo sample hapa kila mtu anufaike,umeomba kitu public weka na hitimisho watu wengine wajifunze na kunufaika.
 
mkuu sikutishi ila hiyo hela hautoirudisha kabla ya pikipiki kwenda gereji kila wiki
Inategemea na uliye mpa mbona siku hizi ndio njia inayotumika sana!!kuliko ile ya hesabu kila siku?kwa mfano kwa dar
mkuu sikutishi ila hiyo hela hautoirudisha kabla ya pikipiki kwenda gereji kila wiki
kwa hili sio kweli kwani ndio njia bora inayotumika sana siku hizi!!mfano dar kila siku anakuletea shilingi 10,000!!kwa muda wa miezi kumi,pikipiki inakuwa yake na lazima aitunze kwani anajua baadaye itakuwa mali yake!!
 
Nashukuru biashara inakwenda vizuri sana kwasababu kijana niliyempa anajitambua na anajua kazi yake anafanya service kila week kwa hesabu yake na anafuata sheria zote za usalama barabarani na chombo kina vibali na document zote kwa mujibu wa sheria.Ni jambo la kumshukuru Mungu sana.
 
Hii biashara kwa mkataba haina faida hata kidogo

Pikipiki inauzwa 2.5 million. Mkataba unaweka wa miezi 10 ambao ni sawa na kulipwa Tsh million 3 (10,000×30×10= Tsh 3,000,000=) kwa mwaka. Na baada ya hapo mkataba unaisha.

Hiyo ni sawa na kwa siku kuingiza faida ya Tsh 50,000/= kwa mtaji wa Tsh 2,500,000/=

Hapo sijaongelea risk kama pikipiki kuibiwa, kupata ajali, kupata dereva kimeo n.k

Hata mkataba ungekuwa wa miezi 12, bado faida itakuwa ni Tsh 91,000/= kwa mwezi, faida hii ni ndogo sana ukilinganisha na mtaji unaoweka. Mimi naona njia sahihi ya kufanya hii biashara bado ni kuletewa kiwango cha siku.
 

Mkuu sidhani kama calculator yako iko sahihi. Hivi 3.6m - 2.5m unapata 91k!?

Hii biashara iko hivi. Unanunua pikipiki ka 2.25m hadi 2.3m (inategemea na eneo/mkoa unakonunulia) kisha unampa dereva wa mkataba kwa miez 12. Kama marejesho yataenda vizuri utapata 3.6m kwa muda huo. Ukipiga hesabu ni kama unafaida ya 1.3 kwa miez 12.
Nakubaliana na wewe kua biashara hii inachangamoto kama zilivo biashara nyingine mfano, kuibiwa, ajali, dereva asiejielewa nk.
Kikubwa ni kuchanga vizuri karata zako na kujitahidi kupata madereva waaminifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…