Kama ambavyo kuna watu waongeaji sana basi kinyume chake kuna watu ambao sio waongeaji hata kidogo,mfano wewe,it's okay ndio maumbile
Lakini pale inapofikia hatua ya kushindwa kuchangamana na watu hata kwa kiasi cha muda mchache hilo ni tatizo,pale unaposhndwa kuonyesha uwezo wako na kikosa morali ya kutumia maarifa ni tatizo
Lakini haya yote yapo kwenye akli yako tu au kwenye mawazo yako na sio hali halisi,kibaya zaidi kile unachoamini ndani ya mawazo yako haijalishi ni halisi au laa ndicho kinachojitokeza kwenye maisha halisi.
Ubongo wa mwanadamu haujui kutofautisha kinachokufurahisha na kinachokuumiza,huwa unafanyia kazi kile ambacho hupewa uzito na fikra zako au hisia zako,sasa utaona kwakuwa unashindwa kuchangamana na watu na kufanya mazungumzo na bilashaka hii hali itakuwa inapewa uzito sana na fikra zako,basi ubongo wako unaona hiki ndio kinachotakiwa kufanyiwa kazi,nacho si kingine ni kukumbusha kwamba usichangamane na watu,usianzishe mada kwakuwa utazingua,usikae na kufanya mazungumzo na watu kwakuwa sio mzungumzaji mzuri
Sasa hakuna kinachoshindikana hapa chini ya jua,hatua ya kwanza ni kurewire ubongo wako na taarifa nyingine tofauti na za awali,kwa kuweka taarifa mpya automatically ubongo utafuta file la zamani na kuinstall file jipya
Anza kufanya yale ambayo yanakupa hofu japo kwa uchache,mathalani unaogopa kuchangia mada,jitahidi kuongea japo kwa uchache,usijali wala kuhofu kuwa je nikiongea pumba watu watanionaje,kumbuka upo kwenye hatua za kuishinda hali hiyo,na tambua kitu kimoja asilimia kubwa ya mambo ambayo huwa tunawaza watu watatuonaje,jua hakuna mwenye muda na wewe,kila mtu ana business zake.
Kwahiyo kadri utakavyo anza kushiriki mazungumzo kidogo kidogo baada ya muda utajenga kujiamini na kuanza kuwa huru dhidi ya hofu na kuwa mwenye kujiamini kwa asilimia Mia moja
Anza hata kuongea au kuchangia mada kwa watu wasiokujua,nenda kijiwe fulani kaa pale kama unavyojua Watanzania huwa tunapiga story hata na tusio wajua,changia pale mazungumzo na utaona jinsi utakavyobadilika,huo sio ugonjwa ni athari tu za kisaikolojia ambazo hutukumba kwenye maisha,labda kutokana na malezi yetu au makuzi yetu