Msaada:Tv kuwaka nakuonyesha logo kisha kutoa mwanga unaofifia taratibu nakua mweusi bila kuonyesha picha

Mtu-people

New Member
Joined
Aug 20, 2019
Posts
2
Reaction score
0
Habari ya jioni wakuu,kuna smart TV inakama wiki inasumbua kuwaka kwa njia ya umeme wakawaida,ilianza ukiiwasha inatokea logo ila rangi ya screen inafifia kama vile umeme ni mdogo kisha baada ya sekunde kama 30 hivi mwanga mweupe unatokea kisha inaanza kuonyesha picha vizuri tu inatilia.Ila leo kila ikiwashwa inawaka logo yenye mwanga wa bluu unaofifia taratibu mpaka screen inakua mwanga mweusi tu sauti unasikiai ila picha hazionekani.
Pamoja na yote hayo,kila ikiwashwa kwa njia ya DC y solar inawaka vizuri kabisa bila kuonyesha tatizo lolote lile.Naombeni kujua shida itakua wapi kabla sijafanya maamuzi yakumtafuta fundi,Itakua ni hitilafu ndani ya Tv yenyewe kwenye mfumo wa AC!?make mfumo wa DC hakuna tatizo unafanya kazi vyema au ni mfumo wa umeme ndio una tatizo linaloleta umeme mdogo?
 
TV yako ina tatizo kwenye mfumo wa Backlight. na kama kwa upande wa DC inawaka vizuri basi ina maana Backlight LEDs zipo sawa na tatizo lipo katika mfumo wa Umeme wa backlight (Backlight Inverter).

Tatizo la umeme mdogo haliwezi kusababisha hiyo shida. Tv inaOperate kuanzia 100v ac hadi 230v au 240v

TV za Kisasa zipo hivi

- Ndani kuna migumo miwili ya umeme ambayo kila mfumo unapotumika kwa kujitegemea ndio maana Picha haionekani lakini sauti inasikika. Kiuhalisia hata picha ipo lakini huwezi kuona kwa sababu kioo kina giza.

Hapo lazima upeleke kwa fundi , kutakiwa na kifaa/vifaa vimeungua kwenye mfumo wa umeme wa backlight.
 
Shukrani mkuu ngoja niufanyie kazi ushauri wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…