Naombeni msaada tafadhali.
Nimenunua eneo la shamba la ekari 4 ambalo nahitaji kulipanda miti ya mbao lote. Naomba kufahamishwa hatua za kuandika proposal kwa aina hii ya mradi na nielekezwe mashirika ambayo naweza kuipeleka ili niwezeshwe kufanikisha huo mradi.Natarajia kufanya shughuli hiyo kuanzia mwezi Nov mwaka huu ili kuwahi mvua za mwakani.
Nitawashukuru sana wana JF ambao watanisaidia kwa ushauri na kunipa changamoto za mradi huo.
Wasalaam!
mh! ni wazo zuri ila naona kama ni ka eneo kadogo...kuwapata investors kwa eneo dogo kiasi hicho ni ngumu kdogo...au unaamnisha proposal ya kupata loan? kwanza eneo lenyewe unalimiliki kisheria? yaani una hati?
Yaani ung-google kwanza interested investors (tanesco wamesinzia, mgololo wana mashamba yao). Jinsi ya kuandika proposal huwa inategemea matakwa ya mwekezaji. Angalia Jatrofa stakeholders in tanzania uone pa kuanzia.
Kila la kheri
Ninafaham namna ya kuandika mirad ila huwez kukurupuka na kutoa msaada,lazma ujue aina ya miti unayotaka kupanda na mambo mengne mengi,TIB wana softloans pale