Mkuu asante sana kwa ushauri wako mzuri.nkuu nakushauri chukua Honda Fit. Ni gari dogo kama swift ila ina nafasi kubwa zaidi ndani na unaweza kupakia mzigo mkubwa sana kwa size ya gari. zile configurations za viti zinakupa uwezo mkubwa wa matumizi yake. kumbuka gari ina kazi sio kukutoa sehemu moja kwenda nyingine pekee. mafuta mimi Napata mpaka 16km kwa lita moja kwa safari za mjini na foleni. Niliwahi kwenda nacho morogoro na kurudi. nilitumia lita 18.5 kwa kutembea km 398 (kutokea bilicanas kwenda mitaa ya jamhuri stadium na kurudi tena mitaa ya bilicanas!) Honda Fit zimeanza kuenea mjini kwa hiyo spea sasa zinapatikana kwa urahisi zaidi. Jaribu halafu utakuja kunambia.
Mkuu asante sana kwa ushauri wako mzuri.
Vipi kuhusu bei ya kununua, ubora katika kudumu kati ya Honda Fit Vs Suzuki Swift?