Msaada ufugaji wa nyuki

Msaada ufugaji wa nyuki

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Habari wakuu. Ninaanza ufugaji wa nyuki kwa hiyo sina uzoefu. Kuna changamoto moja nimeisikia kwamba nyuki wana tabia ya juiacha mizinga na kuhamia sehemu nyingine. Kana hii ni kweli naomba kujua mbinu za kuwafanya wasihame. Natanguliza shukrani.
 
Kama hawatapa mahitaji yao muhimu basi watahama kwenda kuyatafuta kwingine.

Baina mahitaji yao hapafu uwaweze.
 
Habari wakuu. Ninaanza ufugaji wa nyuki kwa hiyo sina uzoefu. Kuna changamoto moja nimeisikia kwamba nyuki wana tabia ya juiacha mizinga na kuhamia sehemu nyingine. Kana hii ni kweli naomba kujua mbinu za kuwafanya wasihame. Natanguliza shukrani.
Karibu kwenye ufugaji wa Nyuki, mimi mwenzio sasa Mwaka wa 3.

Kuhusu kuhama kwa nyuki ndani ya mizinga kuna mambo mengi;
1. Utashi wa Asili WA kutaka kuongezeka na kuzaliana, (Kugawanyika Kwa kundi)
2. Uhaba WA chakula,
3.Nafasi ndani ya mzinga kuwa ndogo mno na kuwazuwia nyuki wafanyakazi kushinda kutekeleza majukumu muhimu kama kujenga masega, kuweka Amina ya Asali na kulea watoto.
4. Kuwepo kwa maadui wa nyuki,
5. Matumizi ya dawa za kilimo ambayo yanadhuru nyuki,
6. Hali ya hewa kama joto Kali, baridi Kali, unyevu mwingj na mvua nyingi,
7. Uvunaji usiozingatia kanuni bora, kuvuna masega yote bila kuwaachia nyuki Asali.

Ukiangalia sababu hizi utabaini chanzo cha nyuki wako kuhama, hivyo itakuwa rahisi kusaka ufumbuzi.

Tunaweza kuwasiliana iwapo shida ni kubwa zaidi, nipo Nyuki Farming Mwanza; Call +255622642620
 
Wenzetu nje wanamkata bawa moja Malkia.anaesababisha Nyuki kuhama ni Malkia.so akiwa awezi ruka akuna kundi kuhama mzinga
Kwa mfugaji wa Kawaida ili aweze kukata bawa Malkia lazima awe na Banjo la Malkia na aweze kumkamata kisha afanye hayo.
Changamoto ni elimu ya Malkia na namna ya kumkamata ili amkate mbawa mfugaji ataweza?

61J04Scps+L._AC_SS450_.jpg

Pichani ni Banio la Malkia ambalo linaweza kusaidia kumkamata Malkia.
 
Habari wakuu. Ninaanza ufugaji wa nyuki kwa hiyo sina uzoefu. Kuna changamoto moja nimeisikia kwamba nyuki wana tabia ya juiacha mizinga na kuhamia sehemu nyingine. Kana hii ni kweli naomba kujua mbinu za kuwafanya wasihame. Natanguliza shukrani.
Karibu tunauza mizinga ya nyuki na makundi ya nyuki
 
Karibu kwenye ufugaji wa Nyuki, mimi mwenzio sasa Mwaka wa 3.

Kuhusu kuhama kwa nyuki ndani ya mizinga kuna mambo mengi;
1. Utashi wa Asili WA kutaka kuongezeka na kuzaliana, (Kugawanyika Kwa kundi)
2. Uhaba WA chakula,
3.Nafasi ndani ya mzinga kuwa ndogo mno na kuwazuwia nyuki wafanyakazi kushinda kutekeleza majukumu muhimu kama kujenga masega, kuweka Amina ya Asali na kulea watoto.
4. Kuwepo kwa maadui wa nyuki,
5. Matumizi ya dawa za kilimo ambayo yanadhuru nyuki,
6. Hali ya hewa kama joto Kali, baridi Kali, unyevu mwingj na mvua nyingi,
7. Uvunaji usiozingatia kanuni bora, kuvuna masega yote bila kuwaachia nyuki Asali.

Ukiangalia sababu hizi utabaini chanzo cha nyuki wako kuhama, hivyo itakuwa rahisi kusaka ufumbuzi.

Tunaweza kuwasiliana iwapo shida ni kubwa zaidi, nipo Nyuki Farming Mwanza; Call +255622642620
unauza asali nchini au soko la nje, kaa ulaya au
 
Back
Top Bottom