Msaada: Ugonjwa wa matikiti maji

Msaada: Ugonjwa wa matikiti maji

Wernery G Kapinga

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2012
Posts
376
Reaction score
127
Jamani mwaka huu niliamua kuwekeza katika kilimo cha matikiti.

Katikati ya safari, kuna ugonjwa umekuja siuelewi. Msaada tafadhali niokoe mkosi huu. Moyo unauma sana maana ni pesa kubwa na mkopo niliwekeza. Msaada wandugu.

IMG_20191022_072437_7.jpeg
 
Pole sana. Mimi nimelima Mahindi gobogobo kwa kumwagilia! Jirani yangu kalima tikiti na limemkubali sana! Ngoja nimuulize.
 
Huo sio ugonjwa bali ni hali inayosababishwa na umwagiliaji wa maji kupita kiasi hasa wiki mbili kabla ya matunda kukomaa.vingine ni joto au umwagiliaji usio na mpangilio

USHAURI
1.Jitahidi kumwagilia kwa mpangilio yaani Kama ni mara mbili kwa wiki iwe hivyo na tena pasipo kuzidisha maji.

2.uwe unafunika matikiti na nyasi huenda ikapunguza kupasuka Kama kisababishi ni joto.

Mengine watajazia wengine,,ila pole sana kwa madhila hayo
 
Kauze buguruni, tandika, mbagara, chanika, yataisha maana wakazi wa huko hawachagui kitu
 
Huo sio ugonjwa bali ni hali inayosababishwa na umwagiliaji wa maji kupita kiasi hasa wiki mbili kabla ya matunda kukomaa.vingine ni joto au umwagiliaji usio na mpangilio
USHAURI
1.Jitahidi kumwagilia kwa mpangilio yaani Kama ni mara mbili kwa wiki iwe hivyo na tena pasipo kuzidisha maji.
2.uwe unafunika matikiti na nyasi huenda ikapunguza kupasuka Kama kisababishi ni joto.
Mengine watajazia wengine,,ila pole sana kwa madhila hayo
Habari,

Unashauri ratiba gani ya umwagiliaji kwa kilimo cha tikiti? Wakulima wengine wanamwagia maji mengi kila siku na kuna wakati maji yanamwagwa mara mbili kwa siku.

Vitu vya msingi kwenye umwagiliaji ni vipi? Nimesoma baadhi ya articles za Wakenya wao wanashauri kumwagilia mara mbili au tatu kwa wiki na matunda yakianza kuwa makubwa unakata kabisa maji
 
Back
Top Bottom