Msaada Ujenzi

BwanaX

Senior Member
Joined
Mar 5, 2015
Posts
123
Reaction score
46
Msaada, naomba kujuwa yafuatayo;

1. Std size ya nyumba ya kisasa
2. Std size ya Master
3. Std size ya public toilet
4. Std size ya sitingroom na dining, kitchen.

NB: nataka nyumba ya vyumba 2 na master1, public toilet n shower, dining, kitchen, store, sitting room.

Asante
 
Hakuna cha standard. Standard unaweka wewe na pia ni function ya pesa yako, na ukubwa wa kiwanja
 
bado hujajibu swali, wacha wenye utahalam wao waje. kiwanja kina 40x40
 
Kwanini usiweke vyumba 3 mkuu,itakuwa poa ila sebule fanya 12×12 na vyumba 10×10 vinatosha...
 
Kuna jamaa humu jamvini anaitwa Jerry akipota hapa atakusaidia. Ukipenda nikuoe namba zake ucheki nae
 
Kuna jamaa humu jamvini anaitwa Jerry akipota hapa atakusaidia. Ukipenda nikuoe namba zake ucheki naeView attachment 250578

Nimependa hio ila kitu kimoja, Nyumba nyingi nimegundua ambazo zina canopy zina fanya rishai au moisture kwa ndani kwa maji ya mvua, Nyumba hupoteza haiba yake, nashauri kutokana na kukosekana material flani au utaalamu wa hali ya juu kwa canopy kutoleta athari kwa ukuta kufanya moisture, bora iyo canopy funika paa kuliko kuweka zege. Just my opinion
 
if u mean standard by "what is recomended to be the minimum" then kuna different values from different angles. ila naomba nikupe mawazo machache.

-writers wameandika vitabu mbali mbali ila zaidi ni kwa ajili ya fixtures, fittings and furnitures.. maana viko directly related to the users.
kwa mfano:standard height ya kuweka urinal kwenye gents toilet ni tuseme 650mm from ground finish level. maana ikiwa juu sana average people hawatafika.

-kuna different proffesional societies/organizations wame recommend such sizes from researches. mfano Un habitat katika makala moja niliwahi soma wali suggest comfortable average space for a bedroom iwe not less than 9sqm. so the sizes can differ from one organization to another.

-ukiwa umempa a proffesional architect kazi yako, moja ya vitu utakavyomwambia ni ur requirements.. mfano its a poor approach to say i need 3 large bedrooms with big windows.. "how big is big, how large is large?"
ila ukimwambia una familia ya 2 girls and 1 boy and a maid. then its ata deal with the sizes accordingly. ur house can have a double bedroom, 2 single bedrooms and a master bedroom.
so bedroom inaweza kua 3m x 4m imtoshe mtu mmoja ila sio watu wa 3.

-incase ulikua unahitaji simple answers labda unahitaji kufanya critic ramani yako nk.. say
:bedrooms zisipungue 12sqm (3mx4m) assumming ni a single 4x5 bed, kabati na ka meza ka kusomea
:lounge atleast 20sqm (4m x 5m) kidogo unaweza piga misele kadhaa
: toilets and shower around 4sqm
:corridors upana 1.2m wide
: jiko similar to bedrooms, with a store maybe ya 4sqm.

sqm- square metre.

-ushauri wa mwisho.. if you are going to spend millions building a home, build right! watumie wataalamu husika.
 

Tumia marumaru ni kiboko yake,maji hayatakaa kwenye canopy
 
Tumia marumaru ni kiboko yake,maji hayatakaa kwenye canopy

Tatizo sio kukaa, tatizo maji yanapo anguka ukuta huroa maji, yaani mvua ikinyesha kwa kipindi kirefu, ukuta unyonya maji na kufanya baridi kwa ndani kupeleka baadaye kufanya ufa, rangi kuchakaa, na kufanya moisture.
 


Mkuu BwanaX kuna mambo mengi ya kuangalia wakati wa ku-design nyumba nitajaribu kuelezea machache kabla sijajibu swala lako.

a) Taste ya mtu...
Pamoja na kwamba kuna standards kama guide lakn bado taste ya mtu ni input mhimu wakati wa ku-design. Mfano mwingine anataka jakuzi kwa bathroom,mwingine hataki, mwingine anataka bedroom ziwe na vitanda viwili vivili, makabati(wadrobes)...n.k n.k

b) Uelekeo wa upepo (wind direction)...
Hii inaleta dhana ya kuamua mashimo ya choo (septic tank na soakaway pit) yakae sehemu gani ya nyumba(vyovyote iwavyo si vizuri kuyaweka mbele ya nyumba)

c) Uelekeo wa jua...
Hii inaleta dhana ya orientation ya nyumba, mara nyingi si vizuri kuweka vyumba vya kulala jua linakozamia, especially master bedroom, ili unapoenda kulala usikute joto liko juu

d) Size ya kiwanja...
Size ya nyumba ni function ya size ya kiwanja, haiwezekani kwa sababu unataka nyumba ya size flani basi ujenge nyumba inayo-cover kiwanja chote bila hata ya kuacha nafasi ya watoto kucheza, it must be designed to well fit in the plot.

e) Functional design/Requirement. ...hapa tunazungumzia uhusiano wa vyumba (connectivity), mfano jiko, dining na lounge havipaswi kuwa mbali mbali sana, na hapa ndipo tunapokuta PRIVATE AREA NA PUBLIC AREA, principally haya maeneo mawili yanapaswa kuwa distinct, yaani akija mtu ambae si sehemu ya familia hatakiwi ajue kirahisi vyumba vya kulala viko wapi na vikoje. Katika ku-fulfil hii requirement inaathiri size ya nyumba.

f) Spacial design/requirement
Sehemu hii designer anajaribu kutumia elimu yake kwa kutumia standards(ulizoulizia) pamoja na taste za mteja ili kupata size za vyumba mbalimbali na hivyo kupata size ya nyumba.

Binafsi ningeshauri nyumba iwe na vyumba vyenye range ya size zifuatazo, size ni katika square metre(sqm)

1.Master bedroom.....14 - 25 plus bathroom/toilet.....3 - 4

2. Bedroom....9 - 14, if is self contained add bathroom/toilet...2.4-3

3. Public toilet. ...2.4 - 3

4. Sitting room. ...22.5 - 36

5. Dining room. ...7.5 - 12

6. Kitchen. ....9 - 16

7. Store....3 - 4.5

Ushauri
Kwa kuwa ujenzi unagharimu fedha nyingi ni busara kupata design nzuri kutoka kwa wataalam hata kama hutatumia wataalam wakati wa ujenzi kuepusha kujilaumu baadae. Ni vizuri pia kujenga katika kiwanja kilichopimwa.
 

Kaka Asante sana umenipa mwanga mzuri sana. nalifanyia kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…