Kuku 3 hadi 4 wanaweza kukaa eneo la SQM 1, yaani hatua moja urefu na hatua moja upana. Sasa banda la kuku 500 unaweza kufanya hatua 15 urefu na upana 8 linatosha kabisa kuku wako hao.
Je unafuga kuku wa aina gani? tunaweza kukupa ushauri bure!!! Kama ni la matofali basi weka kozi 3 tu, then piga waya hadi kwenye bati, hii inasaidia hewa kupita kwa urahisi kupunguza magonjwa hasa mafua.
Jitahidi usafi bandani pamoja na vyombo vya maji kupunguza magonjwa hasa Mafua, Typhoid na Coccidiosis (Kuhara damu)