Msaada: Umeme unatumika sana wakati nina matumizi ya kawaida, tatizo itakuwa nini?

Msaada: Umeme unatumika sana wakati nina matumizi ya kawaida, tatizo itakuwa nini?

Teremaro

Member
Joined
Mar 18, 2022
Posts
29
Reaction score
26
Habari ndugu wana jamii forums, naombeni ushauri kwa wataalam wa mambo ya umeme.

Nyumba yangu ni ya vyumba vitatu, natumia umeme kwenye taa, feni, tv, fridge na heater mara moja moja. Umeme naweka wa elfu 50000 ila haumalizi mwezi!

Pia soma: Vitu vyangu vya umeme vimeungua na umeme wa TANESCO

Kwakweli hiki kitu kinafikirisha sana, naombeni ushauri je, itakuwa ni matumizi ya kawaida? Ama nipunguze nini kinachokula umeme zaidii? TANESCO

Asanteni.
 
jaribu kutafuta chanzo wewe mwenyewe kwanza kabla ya fundi..

zima kila kitu kwa masaa 12 ujue kama kuna sehemu unavuja.

kama hakuna anza kutest kitu kimpja kimoja katika vitu vyako ujue kipi kinakula umeme mwingi. so utaacha labda friji kwa masaa hayo mpaka utajua tatizo ni nini.

iliwahi kunisumbia ila tatizo likawa nyaya za kwenye switch socket hazikuwa zimekazwa vizuri so nikiwasha tv tuu na ndani ya socket panakua na cheche zitokazo. baada ya kukaza umeme ukawa fresh kimatumizi
 
Back
Top Bottom