Msaada unahitajika kwa wajuzi wa sheria

Msaada unahitajika kwa wajuzi wa sheria

iyengamuliro

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
819
Reaction score
366
Habari wana Jf.Niende moja kwa moja kwenye mada.Mimi ni dereva Bajaji na nimekamatwa kwa kosa la kutembea na copi ya leseni kwani orijino ipo na tajiri.Walipo hitaji orijino nikawasiliana na tajiri na ndani ya saa ikaletwa na bado polisi wanalazimisha nilipe faini ya kutotembea na leseni orijino.Je sheria inasemaje kuhusu jambo hili?.Je ni wapi naweza kupata msaada kama mkuu wa traffic anaungana na traffic wa chini yake nilipe?.
 
Naandika kama dereva mzoefu nikiwa barabarani toka mwaka 1996. Umevunja sheria ya kuendesha chombo cha moto bila leseni,haijalishi copy ya leseni unayo na ni copy ya leseni halali ila dereva yoyote kisheria utumiapo chombo cha moto barabarani unapaswa kua na leseni yenyewe na siyo copy ya leseni.lipa faini haraka sana
 
Hiyo leseni ilikua na sticker za uthibitisho kutoka TRA? kama ndio usilipe fine nenda nao mahakamani, kama HAPANA lipa tu mkuu ndo namba hiyo unaisoma, wakati ule traffic angeweza kukuelewesha akakusamehe tu ila wakati huu ni kama traffic wamekua branch ya TRA.
 
Nadhan jamaa wamekujibu vizuri hilo haliitaji mwanasheria , uzoefu unatosha, lipa faini ukawafundishe wenzio
 
Nashukuru kwa michango yenu.Bado nahitaji ufafanuzi wa sheria inayomtaka dereva ambaye hakutembea na leseni awasilishe ndani ya saa 72.Nakama sheria hiyo ipo inatofautigani na kosa langu?.
 
Habari wana Jf.Niende moja kwa moja kwenye mada.Mimi ni dereva Bajaji na nimekamatwa kwa kosa la kutembea na copi ya leseni kwani orijino ipo na tajiri.Walipo hitaji orijino nikawasiliana na tajiri na ndani ya saa ikaletwa na bado polisi wanalazimisha nilipe faini ya kutotembea na leseni orijino.Je sheria inasemaje kuhusu jambo hili?.Je ni wapi naweza kupata msaada kama mkuu wa traffic anaungana na traffic wa chini yake nilipe?.

Njia sahihi ni kukataa kulipa hiyo faini kwao, waambie wakupeleke mahakamani huko ndio utaeleza ishu ilivyo huku ukieleza kuhusu hiyo sheria inayosema upeleke leseni ndani ya masaa 72..
Wanaposema umekamatwa kwa kuendesha chombo cha moto bila kuwa na leseni maana yake ni kuwa hujapewa leseni na mamlaka sahihi (huna leseni halali) na sio kuwa huna leseni hapo ulipo (kwa maana ya kuwa una leseni halali ila hujatembea nayo hapo)..kwa hiyo kama una muda, waambie wakupeleke mahakamani
 
Naandika kama dereva mzoefu nikiwa barabarani toka mwaka 1996. Umevunja sheria ya kuendesha chombo cha moto bila leseni,haijalishi copy ya leseni unayo na ni copy ya leseni halali ila dereva yoyote kisheria utumiapo chombo cha moto barabarani unapaswa kua na leseni yenyewe na siyo copy ya leseni.lipa faini haraka sana
Nauzoefu waio sheria hujui, gari sio uzoefu ndg gari ni sheria katika sheria za barabara hakuna sehemu ya faini kwakutotembea na lesseni

Mleta mada unatakiwa uipeleke original, kama wanadai faini fuata sheria iyo iyo kataa kusaini faini uende kituo husika au ukalalamike kuwa huwezi toa faini kwakua huna kosa.

Wakigoma kama alivosema jamaa hapo waambie nipelekeni mahakamani.

Wengi humu wanaendesha gari kwa mazoea na polisi wanajua hilo.
 
Mpigie kabisa simu umpe maelekezo,kuna kosa la kuiba afu ukipelekwa mahakamani useme nilikua namjaribu tu muibiwa ngoja nimrudishie pesa yake afu unaachiwa hulu
 
mkuu hauko sahihi masaa 72 yanaruhusiwa kisheria hivyo kama alikuwa ndani ya huo muda asilipe ila nje ya muda huo faini inamhusu.
 
Back
Top Bottom