Msaada unahitajika

Mankaa

Senior Member
Joined
Jan 21, 2012
Posts
156
Reaction score
49
Ni kisa kimetokea kwa kaka mmja jiran yangu..kimetushangaza kwa kweli na huyu kaka kaniomba nimshauri nikaona penye wengi haliharibik jambo..

Ni mwaka wa kumi wameoana na mkewe hawakufunga ndoa.wana watoto wawili wa kiume maisha yao yalikuwa yakutokuelewana flani kati ya mume na mke (hata ss majiran tulilifahamu hili) mwaka juzi huyu mume kutokana na kero za mkewe alimua kuoa mke mwingine ambaye hawakufunga ndoa pia wanaishi vizuri na wana mtoto nae mmoja.

Kutokana na huyu jamaa kuowa mke mwingne nyumban kwake pakawa hapakaliki kutokana na fujo na vurugu za huyo mkewe wa kwanza.
Jamaa akaona isiwe shari akampa mkewe mtaji mkubwa tu kaanza kufanya biashara namwanaume kaamishia majeshi kwa bi mdogo kaweka makazi.
Mwaka jana december huyu jamaa alisafiri kikazi nje ya nchi..aliporudi akakuta huyo mkewe mkubwa kaolewa nakijana mdogo kahama na mji kakomba na vitu vyote kaacha watoto peke yao.
Kaolewa na dogo dogo tena mume wa mtu katelekeza mkewe na kitoto kichanga(maelezo ya mwenye mume aliyekimbia)
Huyu jamaa yeye ananiambia hana shida na mkewe huyo lakini je anaweza fanya nini kisheria oli badae huyo mwanamke asijedai chake hapo kwake?kozi kashachukua vitu ndani na mtaji kabeba..

Msaada pls
 
aende kwa mwanasheria atapata maelekezo vizuri,ikiwezekana akaandike RB kwa usalama wake na wa huyo bi mdogo coz anaweza kuja kufanya fujo maana wanawake wengine ni wapenda shari
 
aende kwa mwanasheria atapata maelekezo vizuri,ikiwezekana akaandike RB kwa usalama wake na wa huyo bi mdogo coz anaweza kuja kufanya fujo maana wanawake wengine ni wapenda shari

Kashafikisha polisi na rb anayo
 
Kaa mbali na huyo baba asije kufanya mke wa tatu.
Tilia mkazo ndoa yako kama unayo, kama huna ndoa tafuta wa kukuoa ili uwe bize.
 
kwanza yule rafiki yako vipi....umemsaidia namna ya kupanga matumizi??!!!

kuhusu hiki kisa huyo mke hawezi kusumbua maana keshabeba kila kitu ...kwani alimpa talaka?
 
huyo bi mdogo ameshaishi nae kwa miaka mingapi na bi mkubwa wana watoto wangapi?
 
kwanza yule rafiki yako vipi....umemsaidia namna ya kupanga matumizi??!!!

kuhusu hiki kisa huyo mke hawezi kusumbua maana keshabeba kila kitu ...kwani alimpa talaka?
Mhm..siwez kumsaidia mtu mzima kupanga matumizi coz cjui hata mshahara wake ni kiasi gan.nlichifikiria ni kumwambia tu sina akiniomba omba tena mpaka atachoka mwenyew
 
Bi mkubwa ana watoto wawili bi mdogo wameishi miaka saba

sasa kama bi mkubwa keshahama mji kwa nini aogope ??
ila ni vyema akafuata tartibu za kisheria hasa kuhusu suala la watoto malezi kwani katika kuzungumzia hilo lazima watazungumzia suala la mahusiano yao wazazi ... hivyo aende ustawi wa jamii ili apata ushauri zaidi lakini anatakiwa asimamie kwa suala la watoto na mtengano wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…