Nilitaka kununua nyumba wamiliki ni warithi (nyumba ya urithi) mmoja wa wa warithi wa nyumba hapatikani yuko nje ya nchi lakini ndugu zake watatu walikuwa tayari "tumalize" kila kitu.
Hati zimechekiwa ni sahihi na kila kitu kipo sawa isipokuwa nilisita kutokana na mrithi mmoja kuwa nje ya nchi, hapatikani na hakuna hati yoyote ya kifo chake.
Nimeshaamua kuwa sitainunua kutokana na utata huu, swali je uamuzi wangu ulikuwa sahihi?