Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna watu wengi wametangaza hapa kuwauza ukishindwa google Bena chicks nao wanao aina tofauti tofauti.na wa kienyeji je?
Kwa hawa kuku wa kisasa ni bora ununue kwa makampuni yenyewe au kwa wakala wao hapo Tazara ni madalali hawafai kwa uzoefu tu wanawauzia watu vijogoo au hawa wa kienyeji na utapata hasara, pia vifaranga vyao mara nyingine wazazi hawakupewa chanjo hivyo vifo huwa vingi na huna wa kumlaumu maana ukirudi hukuti mtu. Nenda ubungo mataa pale wanauza wa Mkuza Farm, Interchick au agent wao mabibo opposite na EPZA ulizia hao watakuelekeza. Pia Kenchick wana magari yao yanapaki kila jumanne na Alhamisi nyuma ya YMCA na kuuza vifaranga njoo uulizie. Vifaranga wa kisasa ni bei na kuwalisha gharama ukiuziwa feki ni hasara sana.