Msaada: Upepo kwenye tyres za gari

Mr. MTUI

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
8,130
Reaction score
8,362
Naomba kufahamu haya yafuatayo,
1. Kiasi cha upepo kinachofaa kuwekwa kwenye tyre za mbele na nyuma ( naongelea hzi gari zetu za kawaida siyo malori)
2. Mara ngapi unatakiwa kucheki kiasi cha upepo kwenye tyre na kujaza kwa tubeless tyres.
3. Brand nzuri za tyres
4. Nyongeza: Sport rims nzuri ( na sii ile miogo inayovunjika kwenye humps) zinapatikana wapi
Natanguliza shukrani zangu za dhati
 
upepo mbele 35 nyuma 40, cheki kila baada ya wiki mbili, na unapoenda kucheki gari isiwe imetembea zaidi ya km 2, brand nzuri good year, hapo kwenye sports rim sina uhakika
Unamanisha nn hzo km 2
 
Hizo zote bei zake ni premium aise usijedhan utapata kwa bei 'zetu'. Nadhani kwa gari mfano 265/225/17 ni 490,000/= kwa tairi kwa rim sijui lakini itakua 1,000,000 au zaidi kwa size hiyo
Asee..zinapatikana wap hzo rims
 
upepo mbele 35 nyuma 40, cheki kila baada ya wiki mbili, na unapoenda kucheki gari isiwe imetembea zaidi ya km 2, brand nzuri good year, hapo kwenye sports rim sina uhakika
Kwa gari zote aubinategemeana na gari
 
Tunao miliki baisikeli hapa hapatuhusu wallah.....
 
Mr. Mtui, tairi lolote huwa lina vipimo vya upepo unaotakiwa kuwekwa. Ila kama mdau alivyosema hapo juu bongo tumezoea 35 mpaka 40. Upepo mwingi unaweka sehemu yenye mzigo zaidi.

Lakini pia uwekaji wa upepo unategemea na mzigo uliyopakia kwenye gari.

Mara ngapi unatakiwa kucheck upepo? Hapo inategemea. Lakini standard ni mara moja kwa mwezi. Kama upo Dar, nakushauri uwe unaweka nitrogen badala ya upepo wa kawaida. Nitrogen huwa haipungui kama upepo wa kawaida.

Ukitaka kununua rims nenda msimbazi ukafanye window shopping. Fananisha bei kwenye maduka matatu ndiyo ununue.
 
Kila gari unapofungua mlango wa dereva angalia pembeni kuna sehemu imeandikwa ujazo wa matairi unaonyesha ni kiasi gani unatakiwa ujaze pia inaonyesha kama unapakia watu zaidi ujaze kiasi gani.

Ni vizuri kila unapowasha gari kuangalia matairi yote kwa ujumla kwani huwezi kujua kama ulikanyaga msumari
 
unajuje kama umepungua kiasi kidogo lets say 2psi
 
unajuje kama umepungua kiasi kidogo lets say 2psi
Huwezi kujua kama umepungua kidogo ila kama ni slow puncture utajua tu
Kwa magari mapya siku hizi inaonyesha kwenye dashboard pindi upepo unapo pungua kidogo

Kwa ushauri ungenunua tyre pressure gauge inasaidia sana kuwa nayo
 
upepo mbele 35 nyuma 40, cheki kila baada ya wiki mbili, na unapoenda kucheki gari isiwe imetembea zaidi ya km 2, brand nzuri good year, hapo kwenye sports rim sina uhakika

Km mbili labda uibebe hiyo gari, what i know ni kwamba usiwe umetembea umbali mrefu tairi ikapata moto. Ila si km 2
 
upepo mbele 35 nyuma 40, cheki kila baada ya wiki mbili, na unapoenda kucheki gari isiwe imetembea zaidi ya km 2, brand nzuri good year, hapo kwenye sports rim sina uhakika
Kwanini iwe 35 mbele ma 40 nyuma ikiwa gari yangu sio ya mizigo ni saloon car mfano Toyota Allion. Nifafanulie tafadhali
 
upepo mbele 35 nyuma 40, cheki kila baada ya wiki mbili, na unapoenda kucheki gari isiwe imetembea zaidi ya km 2, brand nzuri good year, hapo kwenye sports rim sina uhakika
Na ni vizuri ukapima asubuhi kabla ya jua kuwa kali kwani hewa ikipata joto huongezeka ujazo na hivyo hutapata vipimo sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…