Mkuu sina msaada wa kukupa pesa ila ninaweza kukuongezea mambo ambayo nadhani ungezingatia
- unapowakilisha jambo, jenga mwonekano wa kuaminika kwa mtu hata ambaye hakufahamu wala hajawai kukuona. mfano nimepitia document yako nzuri kweli imeandikwa kwa lugha safi na inaonesha unauelewa flan wa mambo ya biashara na kuomba mkopo LAKINI jina unalotumia linatisha, kumbuka unaomba mtu akuamini na kukupa pesa zake.( japo najua jina uliweka ili usijulikane wewe nan lakini kuna majna mengi ungeweza kuchagua)
- katika jina la kampuni ni vizuri ungeelezea usajiri wake na kama imewai fanya kazi yoyote inayolingana na plan yako, hii itamsaidia mtoaji wa pesa kujilizisha kwamba nawekeza kwa mtu ambaye kisheria anatambulika. pia kama huwa unanamba ya mlipa kodi husaidia kudhibitisha kampuni yako ni sahihi katika kuwekeza( kama mpya usajir wa brela unatosha sana)
- Pia ungezungumzia ushindani/washindani wako, jekuna huduma kama hio maeneo hayo? kwann wanapeleka dar kwa matengenezo? bei ya dar na mtwara? je utawezaje kuwashawishi wasipeleke dar na kukuamini wewe?. hayo maswali yatampa mtoa pesa uhakika kwamba u mtu sahihi katika hilo.
- katika gharama za kila siku, nadhani ungeelezea matatizo mbali mbali ya simu na gharama za kutatua matatizo hayo, mfano kama simu imekufa screen. screen inauzwa elfu 10 bei ya jumla dukani mimi ntamuuzia mteja elfu kumi na tano na kumuwekea katika simu yake, pia window itanigharimu elfu 50 ila mm ntamuuzia mteja elfu70. hapa unaonesha gharama ya material na lazima ushawishi uwezekano wa kurudisha hio gharama
- katika SWOT ANALYSIS, kipengere cha strength, hapa nilitegemea ungeongelea uzoefu wako wa hii kazi. umewaifanya na kwamuda gani? changamoto za hii kazi na unavyodhibit hizi changamoto. hapa taja makosa ya mafundi wengine ambayo wewe huwezi yaacha yaendelee ili kuwavutia wateja wako, kumbuka strength ziwe za ufanisi wa kazi na kuvutia wateja wakuamin wewe na waachane na wengine.PIA weakness sio lack of capital, taja weakness za kazi hio nini laweza kutokea likaleta madhara/hasara ya bishara. kumbuka unaomba pesa mtu anataka kujua kwamba unajua udhaifu wa biashara hii mfano kunasimu ni ngumu ku by pass password/cloud i.e IOS, au upatikanaaji wa vifaa kama labda nokia x10 kupata display yake unakuaje? na je utafanyeje?
- katika marketing kuna pesa itaitajika hapo hujaeleza hio pesa itatoka wapi maana haipo katka 5m?
PIA NAKUPONGEZA KWA KUFANYA MAMBO KWA USASA HAYA MAPUNGUFU YAKUJENGE NA SI KUKUKATISHA TAMAA.
UNAPOANDIKA PROPOSAL ICHEKI ALAFU JIFANYE WEWE NDIO UNAPESA JIULIZE MASWALI GANI UNGETAKA KUJUA NDIO UYAPATIE MAJIBU KATIKA PROPOSAL YAKO
MUNGU AKUSAIDIE