Wanajamii habarini za mchana,
Nahitaji ushauri wenu katika hili swala limenitatiza sana,mwishoni mwa wiki iliyopita nilipata msiba wa Babu yangu huko kwetu Tanga,na nilipata taarifa jioni ya siku ya jumamosi,nikajiandaa kwa safari kwenda kuwa-join wazazi wangu kwa msiba uliokuwa umetupata,niliwapa taarifa ndugu,jamaa na marafiki kuwa nimepata msiba na jumapili asubuhi nategemea kusafiri ili niwahi mazishi,katika watu amabao niliwapa taarifa ni pamoja na mchumba japo tulikuwa na kamgogoro ka muda mrefu lakini nikaona nimpe taarifa ili asije akasikia kwa marafiki zangu ikaleta shida,nilimtumia sms lakini hakunijibu chochote na ilipofika jumapili asubuhi nilianza safari,mchana kwenye mida ya saa saba ndo nikapokea msg akiniuliza kuwa ni msiba wa nani? na ninakwenda wapi kuzika? nikamjibu ni msiba wa babu yangu na ninakwenda Handeni kuzika baada ya hapo akapiga kimya,lakini nilijiuliza sana kwa nini anyamaze muda wote huo aje aniulize siku ya pili yake,nikaamua kumwuliza jana hukupata msg yangu akaniambia nilipata nikamwambia sawa nikaamua nisiendelee na maswali mengine,nashukuru niliwahi kufika na nikawahi mazishi,na baada ya kukaa huko kwa siku 2 nikarudi maana kazini nilipewa siku 2 tu,kwa kweli wakati narudi sikuona umuhimu wa kumweleza kama narudi kwa sababu hata nilipomweleza nimefiwa response yake sikuifurahia,baada ya kurudi ilipita siku moja na siku ya 2 nilipokea msg toka kwake akilaumu kuwa nasikia tu kwa watu umerudi na ninaelewa kuwa uko mjini na umeshaanza kazi,hiyo kauli pia sikuifurahia nikamwambia hivi wewe hata kuniuliza huko nilikokwenda mambo yameendaje huuulizi unaanza tu kuniambia kuwa unajua niko mjini na sikukwambia kama nimerudi wale ambao ni wa maana kwangu ndo nimewambia nimerudi,kwa kweli nilimwelieza ukweli kuwa sikufurahishwa na jinsi ulivyolipokea tatizo tangu mwanzo kwa hiyo hata wakati narudi pia sikuona umuhimu wa kukueleza kuwa narudi,nilipomjibu hivyo kikazuka kitimtimu huna heshima,una dharau sana,tuachane,nikamwambia kama umedhamiria hayo its fine,nilipomweleza hivyo akaendelea na nitakuja nikushtaki kwa wazazi wako kuwa huniheshimu,nikamwuliza wewe ni kama nani kwangu na kwa familia yangu mpaka uje unishtaki kwa wazazi wangu? na wakati hujajitambulisha na wazazi wangu hawakutambui unaendaje? nilipomwuliza hayo maswali akaanza tena unaona hunithamini,huniheshimu wala hunijali.
Sasa wadau hebu nisaidieni kosa langu hapo ni nini?
Ushauri wenu ni muhimu sana,Nawatakia weekend njema!!