Msaada: Usingizi na uchovu vinanitesa sana

Msaada: Usingizi na uchovu vinanitesa sana

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Siku hizi mwili wangu umekuwa dhofrihali! Siko active kama nilivyokuwa kipindi cha nyuma. Nimejawa na uzembe sio uzembe, mchoko sio mchoko, yaani nipo nipo tu. Nikijiegesha tu, hata dakika haiishi najikuta nshapotea kwenye universe. Jana mchana wakati napata lunch, nimekuja kushtuka ishafika saa 12, boss wangu kamaindi sana. Leo asubuhi nimejiketia tu pale kwenye vyoo vya Umma (PUTO), nimejikuta nishalala kitambo huku mdomo ukiwa wazi

Nowdays hata kwa rikiboy naona uvivu kupitia, replies mbili tu chaaali. Tv ndo ishakuwa adui yangu, hata kabla ya yule mama wa ITV kumalizia muhtasari, nakuwa nshajiondokea kwenye uwepo. Kwenye uchakataji, ile kupima tu oil nishasinzia. Yaani mambo ni vururu vururu

Yaani nimekuwa mvivu sana na mchovu, kutwa kuvuja jasho, hata nipige maji mara tatu, hakuna cha maana. Hapa penyewe tu simu inaniponyoka hivyo! Kwenye kutongoza nikimkaribia tu mwanamke, najihisi uchovu mkubwa sana, naamua kuacha tu

Msaada jamani. Tatizo litakuwa ni lipi?
 
Usiupende usingizi usije ukawa masikini, fumbua macho yako nawe utashiba chakula...
Mithali 20:13
Najitahidi lakini unanizidia. Kuna muda naweka vijiti kwenye kope ili kuzishikilia zisifumbe lakini wapi
 
Fanya mazoezi.
Kula vyakula vya mbogamboga (vegan).
Pia kuwa mtu wa sala.
 
Back
Top Bottom