Msaada: Utaratibu gani naweza tumia ili kurudishiwa VAT

COLINI

Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
12
Reaction score
2
Wakuu, mimi nimesajili jina la biashara yangu, nikapata lesen ya kupeleka bidhaa nje. sasa bidhaa hizo nazichukua kiwandani, wananiuzia na VAT, nikiwaambia mimi na export sitakiwi kulipa VAT hawakubali.

Hivyo naomba kujua hiyo VAT nikisha ilipa pale kiwandani ni utaratibu gani nitumie kurudishiwa hela zangu na TRA? na ni muda gan inatumia mpaka nirudishiwe? kwakweli ina niumiza sana kiasi kwamba wateja wangu nawapa bei za juu hili kufidia hiyo VAT. Sasa kuna uwezekano wakagoma nisaidieni mnao jua tafadhari.
 
Kwanza kabla hujaanza biashara yoyote lazima uwe na uelewa wa mambo ya kodi kwa kiasi haya kidogo.
Watu wengi hata wakiona kipindi cha TRA kwenye TV basi wanahamisha Channel,wakati wanatakiwa kuangalia ili kujifunza.Na wenzio huwa wanaenda pia TRA kupata muongozo.

Ila kwa hili ni Jepesi sana,ni kwamba huna uelewa hata chembe wa mambo ya Kodi na hujui hata TRA wanahusika vipi kwa hizi kodi .
Jibu langu ni fupi tu.Mauzo yawe kiwandani,dukani,mtaani,chooni,lazima kodi ilipwe na wanaokuuzia.
Unapouziwa wauzaji wanakuwa na Record za mauzo ambapo mwisho wa mwezi lazima wapeleke returns TRA ili kujua bidhaa walizouza na makato yake ya kodi.
Na Kwa akili yako ya kawaida hapo unafikiria wewe wapi utalipa kodi?.Na kila mfanyabiashara lazima ailipe.Kinachoonekana hapa ni kukwepa kulipa kodi.Na kuwalazimisha unaowazia kukwepa Kodi ambapo ni kosa la Jinai.
Na Pia hakuna bisahara ambayo haina faida,sasa wewe hadi Kodi unataka iwe faida yako.
Wao wanaelewa ila wewe ndio huelewi,bei wanayokupa ni kwamba ni Tax inclusive Price,ni sawa na unaponunua kibiriti dukani ni kwamba unakuwa umelipa kodi bila kujua,ila baadhi ya biashara kubwa ndio wanaweka na kuainisha kodi kwenye Invoices zao.Na Hapo ndio walipokuchanganya,na ni lazima waanishe hivyo kama biashara nyingine za kawaida tu.

Wengine wataeleza vizuri,maana mie sio mtaalam wa mambo ya kodi
 

unapofanya marejesho ya vat mwisho wa mwezi bidha zako ulizo export zinakuwa kwenye jedwali la zero rated...na ulizo nunu zina kuwa kwenye jedwali la output vat...kwa hiyo kimahesabu utaonekana wewe waidai TRA na sheria inasema waweza claim refund kila baada ya miezi 6...ila tatizo utakapo file for return hakikisha uko kamili maana ndio watakutumia watu wa kitego cha tax investigation n.k
 
Mkuu Zanzibar Spices usiwe mkali. Ukisoma kwenye wwbsite ya wizara ya fedha Tanzania kuna maneno kama haya chini.
That means that all imported products are levied with VAT , while all exported products have no VAT
 
Last edited by a moderator:

Mkuu we ukitaka mambo yawe mepesi basi Shirikisha Kanisa tu ktk hio biashara yako! Mambo yako yatakuwa lainiiiiii.

Hakuna cha kodi wala nini. Jiandae tu kuwa mzee wa Upako kwa sana tu.

Yaani kila atakae kusogelea Unamsamehe madhambi yake.
Utakuja niambia.
 
Nenda TRA ukafafanuliwe mkuu. Tatizo wafanyabiashara wa Afrika wengi hutafuta kila mbinu kukwepa kodi wakidhani ile kodi pia ni moja ya profit yao. Kodi ni mali ya serikali. Mfano: Kodi ya VAT hauilipi wewe mfanyabiashara,bali anailipa mlaji wa mwisho. Wewe ni njia tu ya kupitisha kodi hiyo kwenda serikalini.

Sasa wafanyabiashara,kwa wizi na tamaa tu,huwa wanataka wachukue vyote kwenye bidhaa yaani wakombe gharama ya kitu,faida na kodi ya vat pia. Wewe mfanyabiashara cha kwako ni bei halisi na faida tu. Vat yote ni ya serikali. Ndio shida ilipo. Hata mzozo wa mashine za kodi,ni ujinga na kutaka kuiibia serikali tu ukichunguza kwani kila kitu kinaeleweka.

Wakibanwa sana wanakosa hoja wanasema oh tunalalamikia vifaa vinaharibika mara kwa mara..ha..sasa hii nayo ni hoja ya msingi kweli. Mbona kina coke,pepsi,Tbl,serengeti nk,mafriji yao yanaharibika mara kwa mara kwa wateja wao na wafanyabiashara hao wanachofanya ni kureport na kuita mafundi wa kampuni husika! Kwa nini isiwe hivyo kwa mashine za kodi. Mwisho mkuu narudia tena,nenda ofisi za TRA wakakueleweshe vizuri,usiogope.
 

wewe hapa mtu huyu hujamsaidia zaidi ya kumdharau na kumwambia hajui chochote hata uelewa na TRA, wewe unayejua chochote huu ndo msaada? angekuwa anajua angeuliza? huu siyo msaada ni kama kejeli tu. kiufupi mtu anaye export nje hatakiwi kulipa VAT, anachotakiwa, kule anakofanyia manunuzi atailipa lakini badae kama kweli bidhaa ile ameipeleka nje, atatakiwa kuandika barua ya kudai kurudishiwa ile VAT aliyo lipia kule kiwandani au popote. na TRA ua wanairudisha.

Mimi nimeisha fanya hivyo kwenye kampuni yangu. Kawaida mimi ua naidai baada ya miezi 3 kuisha. nyie ndio mnaonaga wagonjwa wa ukimwi badala ya kuwahudumia, mna anza kuwambia, kwanini uliupata?, kwanini ulizini? nakushauri ukiona mtu anataka msaada ni vyema kumsadia badala ya kunyambulisha makosa yake.
 

mkuu kwenye EFD machines niliona dai 1 la msingi, ambalo ni kulazimishwa kuzinunua kutoka TRA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…