Msaada, uzito wa watoto

binty mzazi

Member
Joined
Jun 27, 2014
Posts
33
Reaction score
8
Wazima humu. Jamani mimi twins wangu uzito wao hata nashindwa kuuelewa, wanakula vizuri tu, wako active lakini kwenye uzito napata mawazo sana. Binti amerudi kwenye kijivu, kijana nae anarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Nisaidieni jamani, nakosa raha sana.
 
wana 10 months, asubuhi tu wakiamka nawapa maziwa, saa 2 nawapa uji wa lishe, wanapumzika, wakiamka nawapa supu ya samaki au mbogamboga itakayokuwepo,wanapumua kama aftr an hour wanapewa juice au tunda wale wenyewe, nikiwa nakunywa chai nao nakaa nao pemben nawapa mkate wanatafuna, mchana wanakula mtori kdg kama starter, wanapumua kidogo wanakula ugali au wali bokoboko, maji kwa wingi wanapewa, wanalala, jion wanapewa cerelac/uji nwa lishe ikiambatana na juice au tunda na maziwa, mida ya saa 1 kuelekea 2 wanakula mtori wa kutosha wanasindikiza na juice au tunda wanalala, ucku wanapewa maziwa yao na mmoja ananyonya mwenzie hataki. Sijui wapi nakosea
 
kifupi wanakula sana, chochote utakachoshika nao wanataka na ukiwapa wanakula. Na ni wachangamfu kweli, binti ni mtundu hadi nahisi kupiga kelele akianza fujo, na ndo kana kilo ndogo sana kuliko mwenzie.
 
kifupi wanakula sana, chochote utakachoshika nao wanataka na ukiwapa wanakula. Na ni wachangamfu kweli, binti ni mtundu hadi nahisi kupiga kelele akianza fujo, na ndo kana kilo ndogo sana kuliko mwenzie.

Wana kilo ngapi? Na mbona kama wanakula sana interval ya kila mlo mbona ndogo. Sema kilo zao uweze kusaidiwa
 
binti 7.1, kijana 7.5 wana 10 months. yeah,wanakula mno.

Ikiwa wanakua vizuri tu na maendeleo yao mazuri tu hakuna shida jaribu kumwona daktari wa watoto,na zingatia kiwango cha damu na maji mwilini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…