Msaada: Vituo Vya Watoto Yatima

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Habari zenu,

Nipo Dar es Salaam na nina misaada nataka kutoa kwa watoto yatima (na pampers labda kwa ajili ya hospitali?) ila sijui pa kwenda. Nahitaji kufahamu ni wapi ninapoweza kupata taarifa sahihi za vituo vya watoto yatima. Kuna ofisi inayoweza kuniambia wapi ninapoweza kuipeleka mwenyewe moja kwa moja?

Natanguliza shukrani.

NB: Mniwie radhi. Inawezekana hii siyo sehemu ya kuweka post ya namna hii ila kiukweli naingiaga sehemu mbili tu humu Jamii Forums - Jukwaa la Siasa na hili la Biashara.
 
Shwari kiongozi!
kwa habari ya misaada kwa watoto yatima na Hospitali kwa maoni yangu ni kwamba katika kila ofisi za serikali ya mtaa kuna kuwa na kamati ya afya na maendeleo ya jamii, hapa ndipo mahali sahihi ambapo utapata taarifa za vituo vya watoto yatima pamoja na hospitali pia, kwa hiyo kila ofisi ya serikali ya mtaa unaowiwa kutembelea unaweza ukapata information unazotaka na watakupa utaratibu wa kufanya.
 

Asante sana. Nitaanzia huko.
 
Kuongezea ,
Nenda ofisi za serikali za kata au wilaya kuna maafisa ustawi Wa jamii hao ndio wanahusika moja kwa moja na hivyo vituo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu akubariki kwa moyo Wa kutoa kwa wenye mahitaji.
A giving pledge........
Waone maafisa ustawi wa jamii wa kata au wilaya husika watakupa details zote za vituo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…