Msaada wa anaefahamu ujenzi wa bwala la kufugia samaki

Msaada wa anaefahamu ujenzi wa bwala la kufugia samaki

ALF

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
207
Reaction score
137
Habari zenu wanajamii. Naomba msaada wenu nina kajieneo ambapo naanza kilimo cha mboga mboga na matunda,pembeni yake nimechimba shimo yenye ukubwa wa 8m kwa 8m kina 2m wazo lakwanza lilikuwa ni kuhifadhia maji kwajili ya kumwagilia na baade kufugia samaki kama kitoweo, lakini kutokana na na sehemu yenyewe kuwa ngumu kufikisha material na uwezo wangu kuwa mdogo nimelazimika kuja kwenye juukwaa hili kuomba msaada wa ushauri wa mawazo kama kuna mtu mwenye ujuzi wa kujua ujenzi wa bwawa hilo usiokuwa wa ghalama kubwa.

Udongo wa huko ni kichanga hivyo hautuamishi maji hivyo ni lazima kujengea kwa zege au matofali, nilitaka kujua je kuna matofali mahususi kwajili ya ujenzi wa mabwawa ya samaki?.kama yapo yakoje?.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
 
Kama uko Dar es salaam unaweza kwenda chuo cha uvuvi mbegani,wizarani(hizi wizara zinabadilishwakila siku sina uhakika lakini ni wizara inayoongozwa na David Mathayo ya mifugo) au kwenye ofisi za wilaya kuna wataalamu wa mambo ya samaki watakuelekeza vizuri
 
Nakutumia simu za watalaam kwa pm, fungua in box yako utakuta simu za watalaam wa FAO.
 
Back
Top Bottom