ALF
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 207
- 137
Habari zenu wanajamii. Naomba msaada wenu nina kajieneo ambapo naanza kilimo cha mboga mboga na matunda,pembeni yake nimechimba shimo yenye ukubwa wa 8m kwa 8m kina 2m wazo lakwanza lilikuwa ni kuhifadhia maji kwajili ya kumwagilia na baade kufugia samaki kama kitoweo, lakini kutokana na na sehemu yenyewe kuwa ngumu kufikisha material na uwezo wangu kuwa mdogo nimelazimika kuja kwenye juukwaa hili kuomba msaada wa ushauri wa mawazo kama kuna mtu mwenye ujuzi wa kujua ujenzi wa bwawa hilo usiokuwa wa ghalama kubwa.
Udongo wa huko ni kichanga hivyo hautuamishi maji hivyo ni lazima kujengea kwa zege au matofali, nilitaka kujua je kuna matofali mahususi kwajili ya ujenzi wa mabwawa ya samaki?.kama yapo yakoje?.
Natanguliza shukrani zangu kwenu.