Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shida zitakufanya usaini mkataba bila hata kusoma. Mwishoe uanze kulia kama mtoto!!Habari za muda wana Jamii Forums,
Samahani na napenda kupata msaada wa kujua gharama za kukodisha eneo kwaajili ya mnara kwenye eneo la mita 30*30 bei imefika shingapi? 2021 hii.
Na mambo gani yakuzingatia kwenye mchakato mzima ikiwepo mkataba.
Asanteni.
Nikweli minara ya simu ina madhara hasa ukiwekwa karibu na nyumba yako?Gharama za kukodisha sehemu za kujenga mnara bei yake ina factor nyingi.
1. Eneo gani? Mjini au kijijini, mkoa gani?
2. Umaarufu wa eneo kukodi kariakoo na sinza ni tofauti.
3. Aina ya mnara unaojengwa
Pia kusema eneo ni 30m kwa 30m hii si kweli hakuna mnara unaokula eneo lote hilo hata kama watajenga BSC au MSC. Ni kubwa mno mzee.
Minara mingu inakaa kwenye 10 kwa 10.
Asante sana kwa majibuShida zitakufanya usaini mkataba bila hata kusoma. Mwishoe uanze kulia kama mtoto!!
Kwanza lazima ujue je kuna madhara ya mnara kukaa eneo (kama ni eneo unapishi).
Pili je unajua nini kuhusu mikataba?
Tatu kama hujui lolote kuhusu madhara ya minara ya simu pamoja na mikataba tafuta wakili aliye sajiliwa akupe ushauri wa kisheria.
NB: Narudia tena, shida zisikufanye usaini mkataba kabla hujasoma utakuja lia baadae.
Pia kuna uzi ulisha elezea hii mada ya kindani pamoja na watu waliolizwa kisa hawajasoma mikataba na kuielewa.. tafuta humu jukwaani upo!
AsanteShida zitakufanya usaini mkataba bila hata kusoma. Mwishoe uanze kulia kama mtoto!!
Kwanza lazima ujue je kuna madhara ya mnara kukaa eneo (kama ni eneo unapishi).
Pili je unajua nini kuhusu mikataba?
Tatu kama hujui lolote kuhusu madhara ya minara ya simu pamoja na mikataba tafuta wakili aliye sajiliwa akupe ushauri wa kisheria.
NB: Narudia tena, shida zisikufanye usaini mkataba kabla hujasoma utakuja lia baadae.
Pia kuna uzi ulisha elezea hii mada ya kindani pamoja na watu waliolizwa kisa hawajasoma mikataba na kuielewa.. tafuta humu jukwaani upo!
Asante sana kwa majibu.Haya mambo sio yakuyaendea kiholela hivi!
Hizi kazi inatakiwa uwe na wakili wako asimamie mchakato mzima!
Ikitokea amekushauri vibaya au kakosea unaweza hata kumshtaki mahakaman na ukapata fidia!
Huyo mteja wako bila shaka anakikosi kazi cha mawakili, consultants na wataalamu kibao ambao wanaweza kutumia legal technicalities ili wajifaidishe wao!
Jipange mkuu, usijejilaumu baadae!
Microwave radiation ina madhara kwenye mwili wa binadamu hii haina upinzani.Nikweli minara ya simu ina madhara hasa ukiwekwa karibu na nyumba yako?
Hongera umejitahidi kuelezeaMicrowave radiation ina madhara kwenye mwili wa binadamu hii haina upinzani.
Lakini madhara ya radiation hizi upungua kutokana na umbali. Mfano wanaofanya kazi juu ya minara inashauriwa usikae mbele ya dishi au antenna inayofanya kazi kama hujavaa vifaa vya kujikinga. Pia ushauriwa kukaa umbali wa mita 2. Sasa piga mahesabu kama mita mbili madhara ndio huwa makubwa. Je kwa mnara wenye urefu wa kwenda juu mita 15 radiation zake mpaka zikufikie uliye chini ni umbali wa kiasi gani?
Conclusion: Madhara yaliyopo ni madogo sana kwa kuwa mnara/vifaa vya mnara vipo juu hivyo nguvu za radiation zinapungua.
Madhara makubwa labda ni noise pollution zitokanazo na generator.....
Nimejaribu kuelezea kwa picha kama utaelewa.View attachment 1694960