Asante mkuu utafiti kwa ushauri wako. Lakini kama una uelewa wowote wa mahali kwa kupata parking devices achana na chupa za konyagi ,ujazo wa lita moja na nusu lita itasaidia sana ,tena zikiwa za plastic maana za chupa ziko so fragile. Msaada wako katika hilo.
Kwa hapa dar kampuni inayoshilia soko sana ni ile wanajiita Tabora Honey ila pia kuna nyengine wanajiita African Queen nao wanakuja vizuri kwasasa maana wameenda mbali zaidi, wana asali zilizochanganywa na karafuu, cinamon na pia zipo za tangawizi.
Kama utapata chupa nzuri yakuvutia asali utauza, bongo biashara yeyote inakubali inategemea na uchakarika vipi.....
Mtafiti narudi kwako tena nimekuwa impressed,maana namie niliwahi kupost pia lakini haikuwa na maleezo ya kutosha,na nimegundua kwamba wale wafanyabisahara wa Asali baadhi yao waliomo JF ndio wana coment negative za biashara hii.
Anyway,Nilikuwa nataka kufanya proccesing mwenyewe,yaani niwe na machine ya kusindika mwenywe,na pia niwe nanua chupa maalum zake zile za kigae.
-Je Mashine za kusindika asali zinapatikana wapi na wastan wa Bei zake.
-Pia chupa zile huwa zinauzwa wapi